Thursday, April 19, 2012

Wanachama 2402 wa CCM Ngorongoro wakiwemo viongozi watimukia CHADEMA

Wanachama wa ccm wakiwemo wenyeviti wa vitongoji vitano wilayani ngorongoro, wametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na chadema,na tayari wamebwaga kadi zao za ccm katika ofisi za chadema zilizopo wilayani humo na kukabidhiwa za chadema.

Tarifa hiyo imetolewa na katibu wa ccm mkoa wa Arusha Amani Golugwa.



Kwamujibu wa katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa, Wenyeviti haowalipiga simu asubuhi ya leo na kutoa taarifa za kuhama CCM. Chadema ilituma KikosiKazi ili kuthibitisha habari hizo na tayari imethibitishwa wanachama hao kuhamaCCM na Kuhamia CHADEMA kama inavyoainishwa hapa chini;

1. Saitabau Tereto - Mwenyekiti waCCM Kitongoji cha Esirwai, 

Amerudisha Kadi yake na kuhamia Chadema, 
Wanachama wengine 478 waCCM katika Kitongoji hiki wamerudisha KADI zao na kuhamia Chadema.

2. Kone Kema - Mwenyekiti wa CCM Kitongojicha Ndiyani, 
AmerudishaKkadi na Kuhamia Chadema,
WanachamaWengine 590 (CCM) katika kitongoji hiki wamerudisha Kadi na kuhamia Chadema 
3. Marko Mbene – Mwenyekiti wa CCM Kitongojicha Ngoyapase,
Amerudisha Kadi na kuhamia Chadema, 
Wanachama wengine 320 katika Kitongoji hiki wamerudishaKadi na kuhamia CHADEMA
4. Saruni Meng'arana – Mwenyekiti wa CCM Kitongojicha Embarware –
Amerudisha kadi na Kuhamia Chadema,
Wanachama wengine 224 katika Kitongoji hikiwamerudisha Kadi zao za CCM na kuhamia CHADEMA
5. RobertEdward – Mwenyekiti wa CCM Kitongoji cha Madukani 
Amerudisha Kadi na kuhamia Chadema,
Wanachama wengine 326 wa CCM katikakitongoji hiki wamerudisha Kadi na kuhamia CHADEMA



CHANZO Arusha Mambo

No comments:

Post a Comment