Wednesday, November 1, 2017

MDUDE NYAGALI AMEKAMATWA NA POLISI

MDUDE NYAGALI AMEKAMATWA NA POLISI

Kamanda Mdude Nyagali amekamatwa na Polisi akiwa ofisini kwake Vwawa, Mbozi mkoani Songwe leo tarehe 01/11/2017 ambapo amepelekwa kituo cha Polisi Vwawa na taarifa za awali zinasema amefunguliwa shtaka la uchochezi na anataka kusafirishwa kwenda Dar au mkoa mwingine.
Japo kwa sasa wamesema madai ya kumkamata ni kuwa ameunganishwa kwenye kesi ya uchochezi ya Mhe. Pascal Haonga (Mbunge wa Mbozi) ya tarehe 28/8/2017 siku ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa mji wa Mlowo pia taarifa nyingine zinaeleza kuwa kesi yake haijafunguliwa kituo cha Vwawa bali ni mkoa mwingine ambao haujatajwa hadi sasa na kuhusu dhamana yake kituoni hapo wamesema inapaswa kusubiri mpaka saa 8 nane mchana huu.

Taarifa zaidi mtazidi kuletewa...
Habari - CHADEMA
Kanda ya Nyasa

No comments:

Post a Comment