Wednesday, November 1, 2017

LIBERATUS MWANG'OMBE AMJULIA HALI MHE TUNDU LISSU HOSPITALI NAIROBI

Katibu wa Tawi la CHADEMA Washington DC, USA ndugu Liberatus Mwang'ombe amefanya ziara ya kutembelea Hospitali ya AGA KHAN Nairobi nchini Kenya kwenda kumjulia hali mwanasheria mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki MHE Tundu Lissu ambaye bado amelazwa baada ya kujeruhiwa kwa risasi alipokuwa Dodoma kwenye vikao vya Bunge vilivyokuwa vinaendelea. Liberatus Mwang'ombe ni mmoja katika watu walioshiriki kikamilifu katika kufanya fund raising ya kuchangia matibabu ya MHE Tundu Lissu kwa kupitia account ya GOFUNDME. Katika zoezi hilo la kuchangia matibabu ya MHE Tundu Lissu Liberatus alishirikiana na Matawi mengine ya CHADEMA ya Marekani likiwemo Tawi la CHADEMA Washington DC, Tawi la CHADEMA Texas, California na pia kushirikisha wanachama na wadau mbalimbali wa CHADEMA waishio Marekani. Mpaka sasa katika zoezi hilo la kukusanya michango zimepatikana jumla ya $32,347 na bado michango inaendelea kukusanywa. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru watu wote duniani kote waliojitolea kidogo walichonacho kuchangia matibabu ya  MHE Tundu Lissu. Mwenyezi mungu awazidishie mengi zaidi ya mlichonacho. Pia tunapenda kuomba wote ambao hawajashiriki kutoa michango yao waendelee kutoa michango yao kwani fursa hiyo bado ipo.No comments:

Post a Comment