Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Morogoro Mh.Suzan Kiwanga, mgombea wa udiwani kata ya Sofi wilaya mpya ya Malinyi pamoja na wanachama wengine 38 wa CHADEMA wakiwa wamefikishwa katika kituo kikuu cha polisi kati, mkoani Morogoro jioni hii.
Hii ni baada ya tafrani iliyozuka baada ya mkurugenzi kujiamlia kumtangaza anayedaiwa kuwa mshindi wa pili kuwa ndiye diwani huku mshindi wa kwanza akiwa amesimama mbele yake. Walipoonyesha kutokubaliana na hilo, walipokea kipigo kutoka kwa polisi na kuwekwa mahabusu katika kituo kidogo cha Malinyi mpaka leo walipopelekwa Morogoro.
Kwa uchache wa pingu, viongozi na wanachama hao walifungwa kamba shingoni na kuunganishwa kwenye machuma ya defender za polisi.
Wakiwa na kamba, walipofika kituo kikuu cha pilisi Morogoro, waliamuriwa kuruka kichura huku wakisindikizwa kwa mateke.
Ili kuhalalisha kukamatwa kwao, viongozi wa kichama na kiserikali waliamua kuwasha moto baadhi ya majengo ya serikali ili kupata sababu ya kuwaweka ndani mbunge na wanachama. Fomu za matokeo zimechomwa moto ili kupoteza ushahidi wa mshindi. Kuelekea 2020 mambo mengi yatafanyika.
No comments:
Post a Comment