Tuesday, October 3, 2017

Mbunge Peter Msigwa awataja waliohusika kununua Madiwani Iringa, vilitumika vifaa vya Australia

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa biashara ya kununua madiwani wa CHADEMA pia ilifanyika Iringa Mjini na kusema kuwa wao walitumia vifaa kutoka Australia kubaini hilo.

Peter Msigwa amesema hayo leo jijini Dar es salaam baada ya kutoka Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambapo walikwenda kuwasilisha ushahidi wa rushwa dhidi ya kununuliwa kwa madiwani hao na wateule wa Rais John Pombe Magufuli.

"Iringa Mjini biashara nayo ilifanyika. Nina ujasiri mkubwa kwamba muhusika mkuu wa biashara ya kununua madiwani Iringa Mjini ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya pamoja na baadhi ya Polisi, hiyo mliona 'Episode' ya Arusha vilitumika vifaa vya Uingereza kule Iringa tulitumia vifaa vya Australia na sisi tutafungua jalada kama ambavyo Mkurugenzi wa TAKUKURU ametushauri.

"Kwa hivyo tusubiri sababu tumekabidhi kwenye korido za Serikali na tunataka sheria zichukue mkondo wake huu uongo uongo wa kusema watu wanaunga mkono utendaji wa Serikali tunataka ufike mwisho ili watu wakae kwenye nafasi zao kwa haki na jinsi ambavyo watu waliamua kuwachagua". alisema Mchungaji Peter Msigwa.

Chanzo: East Africa Radio

No comments:

Post a Comment