Friday, September 8, 2017

Tamko la Umoja wa Ulaya (EU) kufuatia jaribio lililohatarisha Maisha ya Mheshimiwa Tundu Antiphas Mughwai Lissu, Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jimbo la Singida Mashariki

Tamko la Umoja wa Ulaya (EU)

kufuatia jaribio lililohatarisha Maisha ya Mheshimiwa Tundu Antiphas Mughwai Lissu,

Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jimbo la Singida Mashariki

Jumuiya ya Umoja wa Ulaya inatoa tamko lifuatalo

kwa ushirikiano na Mabalozi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya wenye uwakilishi Tanzania

"Jumuiya ya Umoja wa Ulaya nchini Tanzania inaungana na Serikali ya Tanzania, Bunge la Tanzania na mashirika ya kiraia kulaani vikali jaribio lililohatarisha maisha ya Mheshimiwa Tundu Antiphas Mughwai Lissu, Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jimbo la Singida Mashariki.

Jumuiya ya Umoja wa Ulaya nchini Tanzania inaomba mamlaka husika kuwachukulia kwa haraka hatua za kisheria wale wote waliohusika na shambulizi hili lisilofaa dhidi ya demokrasia.

Jumuiya ya Umoja wa Ulaya nchini Tanzania inaungana na watanzania wote kuwapa moyo familia ya Mheshimiwa Mbunge na kuzidi kumuombea apone haraka."





No comments:

Post a Comment