Friday, September 29, 2017

KAULI YA MHE BONIFACE JACOB MEYA WA UBUNGO KUHUSU TUHUMA YA VYETI FEKI INAYOMKABILI MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAMMeya Boniface Jakob amedai Makonda amemtafuta akitaka wamalizane, jambo ambalo analitafriri kama vitisho.

Meya huyo pia amesema ushahidi wote alioupeleka kwenye shauri hilo, haujapingwa mpaka sasa.

Pia amesema ameambiwa na Makonda afute hiyo kesi kwa kuwa naye alikiuka maadili kwa kufanyia vikao vya chama kwenye ofisi yake ya Meya

Amejibu hilo na kusema yeye hakufanyia kikao cha chama ofisini ila alitembelewa na Sumaye ofisini.

Na akahoji mbona Magufuli anafanyia vikao vya CCM Ikulu?

Akasema sekretarieti ya maadili ya viongozi wa uma itaheshimika milele au itadharaulika milele kulingana na maamuzi watakayofanya juu ya swala hilo.

Amesema pia lengo lake sio kumdhalilisha au kumfanya asiwe mkuu wa mkoa ila kuweka rekodi sawa kuwa amefoji vyeti.

Na wanaopinga kuwa anamfungulia kesi wakati Dar ina matatizo lukuki, anahoji mbona kuna watu waliokuwa wanakaribia kustaafu wamefukuzwa kazi na mafao yao yamegubikwa na utata?

No comments:

Post a Comment