Wednesday, June 28, 2017

MAONI YA MAYUNGA

Ndugu wapendwa,

Niwasalimu na niwape hongera kwa kazi mnayoendelea kuifanya.
kwa nini nawapa hongera chadema ? Kwa sababu yote haya ni nyie ndio mnaostahili pongezi na sio hao CCM wanaotaka kupengezana wakati wao ndo wameiletea hii nchi hasara kubwa na umaskini.

Naomba niwape moyo, tena sana. Hao yote na vihoja wanavyowafanyia Chadema ni Dhahiri kwamba wanajua wanatoka 2020. Hivo lazima watawasumbua. Kwa sisi wakristo tunaelewa, ukiwa unatoa pepo, pepo lazima atafanya vurugu, uharibifu, kubambikizia watu kesi, kuharibu mashamba ya watu, kuweka watu hofu, na kitu maana ndo anatoka. Hana silaha ingine Zaidi ya kufungia magazeti na kuto taka ukweli uonekane. Kwa hiyo msivunjike moyo, ndo mafanikio yanakuja hivo, hizo ni ishara ya ushindi unaokuja.
kama CCM wangekuwa hawaogopi kushindwa na Chadema wasingefanya yote hayo. Endeleeni kuwa shupavu na kuwa na msimamo, na kuendelea kuwatendea mema, hata kama wanawachukua. Neena ya Bwana itaanguka kwenu nyie mnapowatendea wema, na kuendelea kuwa waaminifu na kupenda Amani wakati wao wanawachukua. Ushindi ni wa kwetu 2020. Hilo tayari lipo.

La pili na la msingi Zaidi:
Nafikiri mmeona kwamba CCM wanapoteza umaarufu. Na watu wao wengi ni wale ambao hawajasoma, wanawake na watu wasikini. Kwa hiyo tayari ishatupa mbunu Zaidi, na mbinu ni nini ?

a) Tuwatumie wanawake nchini kote na vijijini sasa kuwaelimisha uozo wa ccm. Kuwaeleza ukweli wajue kama sisi ni wapenda Amani na maendeleo. Tuwaambie ukweli wote, na mafanikio ambao sisi tumeyafikia. Hasa tuwa recruit wanawake, kwa ajili ya kuongea na wanawake wenzao kwa sana.

b) Tuwaelimishe watu hasa vijijini mafanikio ya Chadema, na malengo makubwa. Yote ambayo Mhe Lissu kayaongea tuwaweke kwenye elimu wananchi wajue kama sisi nia yetu imekuwa njema muda mwingi ila tumekuwa na siasa mbaya na kunyimwa haki ambayo ingesaidia Tanzania kutoka katika haya tuliyo ingia sasa. Yaandikeni yote vizuri na wawakilishi wetu waaende kijiji hadi kijiji kuelekea 2020.

c) Hao masikini ambao CCM imekuwa ikiwatumia, sasa itawaosa. Tuongee nao na tuwaeleze yote walio ahidiwa yalikuwa ni hewa kwa sasabu ndo kawaida ya CCM wanaomba kura halafu wanawasahau na kuwatenga watu. Waambieni kama mtu hajajifunza mpaka sasa, sisi atajifunza kwa darasa gani maana hali halisi wenyewe wanashuhudia kuwa CCM maneno mengi, ahadi za uongo, bajeti ya uongo, hamna matilizo. Laiti kama CCM wangesikiliza ushauri wa Chadema tusingefika hapa, ila kwa vile CCM ipo kwa manufaa yao hakuna mabadiliko yatayofanyika hata baada ya miaka mingi. Ni yale yale tu.

d) Tuwaelimishe hayo makundi matatu ambayo CCM inapoteza umaarufu, kuhusu katiba mpya na haki zao kama watanzania. Sababu za CCM kupiga chenga katiba mypa ni ili waendelee kupitisha mambo ya ajabu na kutumia nguvu wanaposhindwa. Ni Dhahiri kwamba CCM ni wezi kwa sababu badala kuunda tume ya katiba mpya, wanaunda tume ya kupengezana. Hata hatuelewi wanapongezana kwa nini hasa wakati wao ndo walipiga kura za ndiooo ? Issue ya katiba ambayo ni muhimu, hawaiongelei, walivo wajinga wanapongezana. Haiwezekani wanamwita Mnyika na Wapinzani wezi, wakati wao CCM ndo walipiga kura za ndio. Halafu Spika bado anawapendelea CCM. Upuuzi kweli kweli asee. Hatujawaji kuona unjinga kama huu, ni Tanzania peke yake tu.

e) Kwa hiyo msifedheheke, hao watanzania wanaowapigia makofi CCM, msisahau kwamba wasio kuwa na elimu wengi ni CCM. Kwa hiyo isiwa shangaze wao kupongezana hata kwa mambo ya kijinga. Hiyo pia itaelezea Bashite aliyefeli hawajaona ni tatizo, kwa sababu wote inawezekana hamna kitu. Kwa sisi tusiwalaumu wananchi, tuwafungue akili. Manake waliohakikisha hawapati elimu ni hao CCM. Ila sisi tuendelee kuwafungua akili watanzania kila kona vijijini.

Tukumbuke ya kwamba hakuna chama kilichotowala madarakani forever. Hakuna hata kimoja duniani. CCM inatoka 2020, ndo mwisho wao. Wao ni binadamu kama sisi, wanashindwa hoja sasa ndo maana umaarufu unapungua. Huyu JPM was their last shot, baada ya huyu 2020 hamna mwengine. Tena kesha haribu vya kutosha kwa kuto kuwa na utawala wa sheria na mengi kapindisha. Hata wenyewe ndani kwa ndani sasa hivi CCM wamegawanyika. Sasa kama wenyeye kwa wenyewe wamegawanyika inamaana ndo mwisho wao huo 2020.
Kwa hiyo endeleeni na mapambano ya Amani, haki, kweli, na uzaelendo wa kuwaelimisha wananchi na haki zao. Ubabe wao hauna kitu kwa sababu hauwezi kushindana na watu wanaopenda Amani na haki wa sisi wa chadema. Ndo maana kila siku wanatuonea lakini ndo wao wanaopungua nguvu kila siku. Na magazeti yote wafunge lakini ukweli mbele za Mungu hautafichika, utabaki kuwa ukweli. Wanatanzania wanaanza kujua ukweli, na kweli itawaweka huru 2020. Keep reaching out to all the people of Tanzania, in all corners of the country.
Kumbukeni, Goliath alikuwa Mkubwa na anatisha kwa David. Lakini David akasema huyu na ukubwa wake wote, ntamwangusha tu. Na kweli akaangua na hakuna alie amini.

Kwa hiyo na nyie Chadema msiangalie ukubwa wa CCM au vitisho vyao, watang'ooka tu !
Shetani silaha yake kubwa ni vitisho na hofu, kunyima mtu haki.

Hivo Endeleeni na kazi yenu ya kuwafikia watanzania wote nchi nzima wajue uongo wa CCM na kulindana kwao wanapofanya maovu kwa nchi.

Bwana awabariki sana viongozi wetu, tuko pamoja kabisa. Tanzania itafanikiwa chini ya uongozi wa chadema, na uongozi unakuja 2020.

People’s Power !

No comments:

Post a Comment