Wednesday, June 28, 2017

MAONI YA JUSTIN PHILIPO

People’s Power !
Ndugu zetu watanzania na wana Chadema,
Tunawasalimu sana kwa upendo.

Tunaomba muangalie hii kauli ya Mhe Rais. Tunashindwa kuelewa hizi siasa za CCM zitaisha lini kwenye mambo ya maendeleo. See attachment, gazeti la ITV online leo kwenye facebook yao.

Hivi Raisi anataka sisi wazalendo (DIASPORA) tuje tuwekeze bila vibali ili baada ya hapo watuite wezi au ??

Kama kweli ana nia nzuri ya kufungua viwanda vingi si apelike hili swala bungeni DIASPORA wapewe Dual Citizenship ili wafanye haya maswala ya maendeleo kisheria kwa KATIBA MPYA.

Kwa nini anataka tufanye bila kufata sheria ? Si ndio mambo haya ambayo Chedema wamekuwa wakiyapigia kelele kila siku kwamba tupitishe sheria ya DIASPORA ili maswala ya maendeleo yafanyike.

Kwa nini hawa CCM wanapiga ndio mambo ya kipuuzi bungeni lakini kama haya maswala ya muhimu hawawaungi mkono Chadema?
Tunaomba muwaambie bungeni hao wapuuzi wa CCM kama wana nia nzuri ya kuanzisha viwanda, basi wawaunge mkono nyie wa Chadema ambao kwa miaka mingi mmekuwa mkidai katiba mpya na sheria ya kuwalinda DIASPORA zipitishwe kwa mambo ya maendeleo kama haya.

Waache kutumia wingi wao kwa mambo ya kipuuzi na waangalie kupitisha sasa mambo ya maendeleo. Maana DIASPORA hatuwezi kufanya kitu cha maana bila sheria kuwa sawa. Hatupendi kuvunja sheria, na tunajua ndo nia ya CCM kukiuka sheria mda wote na kunyang’anya watu mali zao baadae na kuwaharibia na kuwaita watu wezi.

Watu wa DIASPORA (wazalendo anaowaita Raisi kwenye article hii) hawawezi kuchukua credit zao nje ya nchi kuja kuwekeza kama wazalendo, kama sheria hazieleweki. Maana wasije baada ya mda wakaja kutuambia sisi ni wezi kama ACACIA wakati waliotuambia tufanye bila kufata vibali ni wao serikali wenyewe.

Tunaomba Waheshimiwa Wabunge wetu wa Chadema muendelee kuwaeleza Dual Citizenship ipitishwe Bungeni kama Chadema walivokuwa wakidai miaka yote bungeni kwa Katiba Mpya. Kwa ajili ya maswala ya maendeleo kama haya. Hii kufanya vitu bila vibali kama anavotaka Mhe Raisi kwenye hii article sio busara na sio utawala bora wa Sheria ambao hata sisi watanzania hatukubaliani nao.

Kwa nia yenu Chadema mnayoionesha ya kusimamia haki, ukweli na maendeleo, tunaendelea kuwaunga mkono na tutahakikisha mnaingia madarakani 2019 and 2020 na kuchukua viti vya ubunge.

Watanzania tumechoka na siasa, bageti hewa zisizofikiwa malengo, na ahadi za uongo za CCM.

Kuna msemo wa Kiswahili unasema, za mwizi ni arubaini! CCM arubaini zao zinaishia 2019 and 2020!

People’s Power 2020!

~Justine Philipo

No comments:

Post a Comment