Wednesday, May 24, 2017

Msahama wa Kodi kwa kufungua viwanda, maandalizi mabovu ya utekelezaji wa kuwaondosha wenye vyeti feki, Katiba Mpya

Wapendwa,
Kwanza tupeane pole kwa yaliyotokea Arusha. Bwana akawape nguvu famililia zote zilizopatwa na janga hilo, pamoja wa nyie viongozi wetu katika kuwafariji wafiwa.
Sasa tuje kwenye siasa za hii serikali mbovu ya CCM:

Tunaona Mhe Rais anasema yuko tayari kutoa msamaha wa kodi kwa watakao fungua viwanda.

Tunaomba muwaelimishe hao ccm waliokuwa na uelewa mdogo wa kujua kusoma na kuandika tu kwamba:

Uchumi umedorora kwa sababu mzunguko wa pesa ni mdogo, wakulima wana hali mbaya (vifaa kwa kilimo ghali bado), biashara zinafungwa hata ukijenga utamuuzia nani ? Kama biashara zote serikali inafanya tu na taasisi zake tu, basi wakubali pia hizo taasisi ndo wawe pia wateja wa viwanda hivyo.

Kwa mfano: Shughuli nyingi za ulinzi zinafanywa na suma JKT, ujenzi Suma JKT na TBA, ndege wapande za ATCL, mikutano na makongamano wanafanyia kwenye taasisi za serikali, benki NMB tu, matangazo TBC na magazeti ya serikali tu. Kwa system hii hatutafika mbali. Ni sawa kutoa pesa mfuko wa suruali unahamishia mfuko wa shati ! Makampuni mengi yameshindwa kumudu hali hii, wafanyakazi wao wameachishwa au kupunguzwa.

Sio kweli kwamba kila anayesema hali ngumu alikuwa mpiga dili, wengine hata namna ya kupiga dili hatujui!!

Serikali iruhusu shuguli zake kufanywa na Taasisi binafsi, kampuni za watu binafsi, au hata watu binafsi na wawekezaji wan je, na msingi Zaidi watu wa Diaspora ambao bado ccm inawaletea siasa nyingi badala ya vitendo walivoahidi. Ndo mambo yanayo changia kuzorota uchumi.
Ni ngumu kumwambia mtu wa Diaspora aweke pesa kupata msamaha huu wakati hamna kitu kilichopo kisheria, kilichopitishwa bungeni kumpa hiyo status ya kumlinda kibiashara.

Kesho au keshokutwa wakisema msamaha wa kodi umeisha halafu umefungua kiwanda na bado status hazijarekebishwa, watu wata poteza pesa zao kwenye uwekezaji.

Kwa mtazano wa economics ni risk na serikali hawezi kumpata mtu kuweka pesa nyingi kwa sababu tu ya hiyo danganya toto ya msamaha wa kodi.
Kwa hiyo hii misamaha ya kodi ije wakati taasisi binafsi zinaendesha uchumi sio serikali kutaka kufanya kila kitu.

Ndiyo haya mambo Mhe Lissu, Mbiliyi na Wabunge wa Chadema na UKAWA mliyasema kwamba haiwezekani tukawa na Viongozi wanaojua kusoma na kuandika tu.

Ni sahihi mlivosema; kwa sababu kama wao serikalini hawaoni haya basi wanajua kusoma na kuandika tu.

Ndo maana hata KATIBA Mpya wanaichelewesha bila msingi kwa sababu wengi CCM utakuta ni wale wa kusoma na kuandika tu, hivo wana mawazo finyu, na hawatoweza kujua principals za economics/ world economics, na madhara ya kuchelewesha katiba mpya kwenye maswala ya uchumi na maendeleo.

Ni Tanzania peke yake dunia nzima ambayo imetumia mabilioni hayo kwenye katiba mpya halafu raisi anasema sio priority.

Jibu Zuri Mhe Mbowe:
Mwisho, nimpongeze pia Mhe Mbowe kwa kujibu vizuri swali la Mhe Raisi. Aliahidi Bilion 1.3, zimiefika Milion 300 tu. Maana ndio kawaida ya CCM kupenda kutaka kuwafanya wapinzani waonekane wabaya. Ila mbinu zao hazitafanikiwa. Uzembe ni wa CCM ila wanataka kuwafanya wapinzane waonekane wabaya. Endeleeni kuwaumbua hivo hivo,mbinu zao na utapeli wao hautafanikiwa. Kama Mhe Mbilinyi majuzi alisema Mbeya Chadema wamejenga madaraja 10 ndani ya miaka 2, wakati CCM hawajafanya kitu tangia tupate uhuru.

Serikali kukata umeme Arusha kwenye taasisi za serikali:
Hatujapendezwa na kitendo cha serikali kuruhusu TANESCO kukata umeme kwenye Hospitali za serikali na Polisi. JKT hawana umuhumu sana. Ila Hospitali za taifa na Polisi wanahitajika muda wote. Hivo badala ya kununua ile Ndege ya Dreamliner kwa malipo ya jumla (cash), basi serikali ingelipia deni la Hospitali na Polisi maana haya ndio mambo ya huhimu kuliko hiyo ndege.

Vyeti Feki:
Kama serikali ilikuwa inajua kupitia Wizara kama watafukuza watu, kwa nini Wizara nyeti kama ya Afya haikuji andaa na upungufu utakao tokana na watu kuondolewa kwenye hospitali za serikali ? Madhara yake kuna hospitali na zahanati mikoani imebidi zifungwe kwa sababu hakuna wahudumu. Kwa nini hawakujiandaa mapema na matokeo wakati walijua huu ndio mpango wao?

kwa nini sisi wananchi tuadhibiwe kwa kukosa huduma za afya mikoani kwa uzembe wa serikali CCM ya kutojiandaa na matokeo ya kuhakiki na kuondosha wafanyakazi wa umma kwenye hospitali za serikali ? Tunaomba Muiwajibishe Serikali, na wekeni yote kwenye rekodi ili muwakumbushe wananchi muda wa chaguzi zote.

Hatuelewi CCM wana matatizo gani, ila inawezekana kwa sababu ya kujua kusoma na kuandika tu ndo maana hawaoni mambo mengi ya maana. Maana mambo wanayoyafanya CCM siku zote hayana manufaa au umaarufu kwa wananchi wa Tanzania waliopo ndani na waliopo nje ya nchi.

Watu wanataka Katiba mpya wao wanaleta siasa huku tumetumia mabilioni ya pesa ya sisi walipakodi zimepotea.
Watu wanataka utawala wa sheria na uongozi bora, wao wanawakinga hawalifu kama wakina Bashite.
Watu wanataka watendaji kuwa na elimu ili kuwa na mtazamo ukubwa kiuchumu, wao wanataka kujua kusoma na kuandika tu. Mpaka kuna siku tutakuja kuwa na Wizara Ya Afya na Science na Technologia zenye Engineers, Doctors, Economy and Financial Proffesionals itakayo kuwa inapewa amri na wakina Bashite

Hawa CCM sijui wana matatizo gani !

Tunawashukuru Chadema na UKAWA endeleeni na kazi nzuri bungeni, huwa tunasikiliza mapambano yenu kwenye "chadema in blood" na online hapa na tunaendelea kuhakikisha jitihada zenu zinawafikisha ikulu 2020 ambapo mnapo stahili kuijenga Tanzania kwa vitendo. Maana hii miaka 55 ya CCM sasa inafika mwisho.

Tuko pamoja.

Na Steven Mayunga

No comments:

Post a Comment