Wednesday, May 24, 2017

Meya wa jiji la DSM kusaidia deni la Makaburi ya Tambaza

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameahidi kusaidia kupunguza deni la sh. Milioni 16 linalodaiwa na mkandarasi wa kampuni ya Ushirombo kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa makaburi ya Tambaza.

Meya Isaya alisema kuwa kwa nafasi yake atajitahidi ili kuhakikisha kwamba anasaidia kupunguza deni hilo kama sio kumaliza kabisa kutokana na umuhimu wawatu ambao wamepumzishwa katika eneo hilo.

Meya Mwita aliyasema hayo jijini hapa jana wakati wa dua maalumu ya kumuombea Sheikh Yahya Hussein sambamba na kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema kwamba hafanyi jambo hilo kwa ajili ya mambo ya kisiasa ama kuwafurahisha waisilamu, bali ni kutokana na kutambua umuhimu wa watu waliolala katika eneo hilo, hasa ukizingatia kila mwanadamu lazima apitie hatua hiyo.

“ Nimesikia kwenye risala yenu kuwa mnadeni ambalo nikubwa, lakini mimi sitasema nitachangia kiasi gani, ila nitapunguza kwa nafasi yangu kiasi ambacho mnadaiwa” alisema Meya Mwita.

“ Watu ambao leo hii tunawakumbuka wamelala hapa, walikuwa na mchango mkubwa , kila mmoja anatambua hilo, waliweza kuitangaza nchi yetu kwenye mambo ya dini , lakini pia kwenye mambo mengi ya kimaendeleo , hivyo tunatakiwa kutambua na kuwakumbuka” aliongeza.

Aidha katika hatua nyingine , Meya Mwita aliwasihi waumini wa dini ya kiisilamu , katika kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuwaeleza kwamba ni muhimu kuendeleza mambo mema ambayo huyafanya wakati wa mfungo huo.

Alifafanua kwamba , imekuwa ni kawaida kwa mwisilamu kutumia kipindi cha mfungo wa ramadhani kuficha maovu na kutenda mema ,lakini baada ya kumaliza kipindi hicho huendelea na matendo yasiyompembeza muumba wao.

Alisema ifike wakati kwa kila muumini ,kutambua umuhimu wa kutenda na kuendeleza mema ambayo aliyafanya wakati wa mfungo kwani kufanya hivyo kutamuweka kwenye nafasi nzuri ya kiimani.

“ Kunajambo ambalo ndugu zangu waisilamu huwa mnafanya, wakati wa mwezi kama huu ambao tunaelekea, kila mwislamu utamuona akihusisha kwenye mambo mema tu, ale ambao walikuwa hawaswali wataenda msikitini, wale ambao walikuwa wakitenda mambo machafu ya kumchukiza muumba wao wataacha”

Lakini baada ya kipindi hicho cha siku 30 kumalizika kila mmoja atarudi kwenye tabia yake, sasa hili jambo ni mtihani kwakweli, niwasishi tu, najua naongea maneno machungu , naninawagusa wengi, tujenge utamaduni wakuyaendeleza haya badala ya kuacha” alisisitiza Meya Mwita.

Hata hivyo Mashehe waliohudhuria dua hiyo, walimpongeza Meya Mwita kwakuwa na moyo wa kujitoa kwenye shuguli za kijamii na hivyo kumuomba kuendelea na misingi hiyo ili aweze kuwatumikia vizuri wananchi wa jiji analoliongoza.

No comments:

Post a Comment