Monday, October 3, 2016

MEYA WA DAR ES SALAAM AWATAKA WAZAZI KUTUMIA MUDA MWINGI KUWAFUNDISHA WATOTO WAO MAADILI MEMA

WAZAZI wametakiwa kutumia muda mwingi kuwafunisha watoto wao maadili mema ili kuepuka kuwa na Taifa lenye watumishi ambao hawana maadili.kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wakati wa mahafali ya wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Amkailiyopo Kigamboni jijini hapa.

Isaya alisema watoto wanapomaliza shule huwa na tabia nje kutokana na maadili ambayo anafundishwa na walimu wao wakiwa shuleni lakini wazazi wanashindwa kuendeleza nizamu zao na hivyo kujikuta wakijiingiza kwenye makundi yasiyokuwa na
maadili.

Alisema wanafunzi ambao wanamaliza elimu ya msingi ndio wanategemewa na Taifa kuwa viongozi wa badae na kwamba kama wazazi wasipotunza nidhamu za watoto taifa linaweza kukosa viongozi ambao hawana maadili." Wazazi tusaidiane, kutunza nidhamu ya watoto wetu, walimu wanajitahidi kuwafundisha maadili mema,na hawa ndio viongozi wetu,hakuna wengine kama
tutashindwa kutunza hiki ambacho wamekipata kutoka kwa walimu ni dhahiri kwamba tutakosa viongozi wenye maadii na Taifa kulipeleka sehemu mbaya" alisema Isaya.

Akizungumzia shule ,Isaya alisema imefika wakati sasa kila mzazi aone umuhimu wa kujenga shule za kata kutokana na kwamba bado serikali inajukumu kubwa la kuhakikisha kwamba shule hizo zinakuwa bora kama ilivyo kwa shule ambazo zinamilika na watu binafsi.

Alisema anafahamu kwamba wapo watu ambao wanauwezo wa kuisaidia serikali badala ya kusubiri kila kitu kifanyike kupitia serikali na kwamba kwakuisaidia itakuwa ni njia moja ya kujenga Taifa ambalo linajali maendeleo ya wananchi." Tuwe na utamaduni, leo hii ukipita nakuona kwamba kuna shule ambayo hainamadarasa ya kutosha, ukanunua mabati kadhaa ukapeleka utakuwa umesaidia watoto ambao wanasoma pale badala ya kusubiri serikali ije kufanya, nayo ina mambo mengi" aliongeza.

Hata hivyo Meya Isaya aliahidi kuchangia shule hiyo Kompyuta tano hatua ambayo ilitokana na risala iliyosomwa ambayo ilieleza kuwepo ka mkakati wa kujenga chumba cha kompyuta kwa ajli ya kufundishia wanafunzi. sambamba na hilo, alisema kwamba anafahamu mchango unaotolewa na shule binafsi na kwamba hiyo ni changamoto pia kwa shule za serikali kufanya vizuri kwenye mitihani yao kama ambavyo inatokea kwenye shule hizo.

Awali akimkaribisha Meya wa Jiji , Meneja wa shule hiyo Dk. John Makoa pamoja na mambo mengine alimpongeza kwa kuchaguliwa kuwa meya wa jiji na kusema kwamba anatambua juhudi zake za kufanya kazi na kwamba wananchi wa Dar es Salaam wanatakiwa kujivunia kupata kiongozi kama yeye.

No comments:

Post a Comment