Katika kikao walichofanya jana, UKAWA walipitisha maazimio kukabiliana na mgogoro unaoendelea ndani ya CUF. Maazimio hayo ni pamoja na;-
1. Hatumtambui Prof. Lipumba kama mwanachama wa CUF na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA
2. UKAWA wanautambua uongozi wa Julius Mtatiro na Maalim Seif
3. Wanachama wa vyama vinavyounda UKAWA wasitoe ushirikiano kwa Prof. Lipumba na washirika wake
4. Wenyeviti wa mitaa, vijiji, Madiwani, Wabunge wasitoe ushirikiano kwa Prof. Lipumba na washirika wake
5. Wabunge wote wanaomuunga mkono Prof. Lipumba watatimuliwa ndani ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
6. Ushirikiano wa kisiasa Tanganyika na Zanzibar utashughulikiwa na UKAWA
7. Mawakili wa UKAWA watamfunguliwa mashtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kwa matumizi mabaya ya madaraka na
8. Mawakili wa UKAWA watamfungulia mashtaka Prof. Lipumba.
No comments:
Post a Comment