Wednesday, October 19, 2016

KATIBU MKUU WA CHADEMA ALAANI TUKIO LA RC GUMBO KUMZUIA MBUNGE GODBLESS LEMA KUWEKA JIWE LA MSINGINimesikitishwa sana na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kuvuruga sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya huduma za mama na mtoto.

Si tu kwamba ameonyesha kukosa staha kwenye jamii, pia ameonyesha kutounga mkono mahitaji ya nchi na dunia nzima "hasa kwa mahitaji ya akina mama na watoto"

Nalaani tabia hizi za kihuni zisizo na tija kwa Taifa. Ikumbukwe tu kwamba; mwanzo wa ngoma ni lele. Tabia ya Mkuu huyu wa mkoa inajenga chuki na yaweza kuleta machafuko yasiyo ya lazima. Mtu wa hivi hafai kabisa katika jamii

Tumpinge!
Katibu Mkuu Chadema Dr Vicent Mashinji.

No comments:

Post a Comment