Monday, June 13, 2016

Mbowe ashikiliwa na polisi kwa kosa la kusalimia wananchi

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Vijana Taifa Patrobas Katambi, Katibu Mkuu wa Vijana Taifa Julius Mwita, Mbunge wa Tunduma Frank Mwakajoka, viongozi wengine wa chama na wanachama wengine, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo cha Polisi Nyakato, jijini Mwanza.
Hadi sasa hakuna maelezo ya sababu ya kushikiliwa kwao. Tangu asubuhi Mkiti wa Chama Taifa Mbowe na alikuwa akizunguka katika maeneo kadhaa ya jijini Mwanza kuwasalimia wananchi katika 'vijiwe' mbalimbali jijini humo.

Tumaini Makene
Ofisa Habari Chadema Taifa.

No comments:

Post a Comment