Saturday, January 16, 2016

Ukawa waongoza Manispaa za Ilala, Kinondoni

HATIMAYE baada ya danadana za muda mrefu, uchaguzi wa kuwachagua Mameya wa Manispaa za Kinondoni na Ilala, umefanyika na Umoja wa Vyama vinavyodai Katiba ya Wananchi (Ukawa) wamefanikiwa kuongoza Manispaa hizo. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).


Chaguzi hizo zilizhairishwa mara mbili kutokana na mvutano uliotokewa katika chaguzi za nyuma, ikiwa pamoja na kusimamishwa kwa amri za mahakama.

Kwa upande wa Manispaa ya Kinondoni, Diwani wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema, Boniface Jacob amefanikiwa kuwa Meya wa manispaa hiyo baada ya kushinda kwa kura 38 dhidi ya mpinzani wake, Benjamin Sitta wa CCM aliyepata kura 2o. Naibu Meya ni Diwani wa Tandale kwa tiketi ya CUF, Jumanne Ameir Mbunju.

Uchaguzi wa Manispaa ya Ilala ambao leo pia uliingia katika mgogoro kati ya madiwani wa CCM na wale wa Ukawa, hali iliyosababisha CCM kususia uchaguzi huo na kuwaacha Ukawa kupiga kura peke yao na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kumtangaza mshindi kuwa Meya wa Ilala ni Charles Kuyeko (Chadema) amepata kura 31, wakati Naibu Meya ni Omary Kumbilyamoto (CUF) amepata kura 31.

Jumla ya madiwani waliotakiwa kupiga kura katika uchaguzi huo ni 54, hivyo madiwani 31 wa Ukawa waliobaki ndani walitimiza akidi ya uchaguzi huo kuendelea.

No comments:

Post a Comment