Sunday, January 31, 2016

Meya wa Chadema kuanza na kero sugu Ilala

WIKI mbili tangu kuapishwa kwa madiwani wa Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko ameanza kazi kwa kutembelea Kata zote zilizopo Ilala na kuanza kukabiliana na baadhi ya kero za muda mrefu. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).


Diwani huyo wa Bunyokwa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema , yeye pamoja na Naibu Meya wake, Omary Kumbilamoto Diwani wa Vingunguti (CUF) wameshaanza kufanya ziara za kutembelea masoko maeneo ya machinjio.

Amesema moja wapo ya kero kubwa inayohitaji kutafutiwa ufumbuzi wa haraka ni Daraja la Mongo la ndege lililo sombwa na maji na kuwaacha wananchi kuendelea kutaabika

“Daraja hilo limekuwa ni kero kubwa kwa wakazi wa eneo la Ukonga tangu limeharibika ni miaka miwili mpaka sasa halijapatiwa ufumbuzi huku wananchi wakiendelea kuteseka” amesema Kuyeko.

Amesema katika kipindi hiki kifupi tayari tumeshawafikia wananchi na kusikiliza kero zao na nimewaahidi kuyashugulikia kama nilivyo waahidi wakati wangu wa kampeni

Amesema, kwa sasa anajikita zaidi katika ukusanyaji wa mapato katika Wilaya yake hii inaendana na kubuni, kudhibiti na kuongeza vyanzo vya mapato ili kupata uwezo wa kuzitatua kero za wananchi.

Aidha amesema kuwa, Februari 6 mwaka huu kutakuwa na mkutano wa Baraza la Madiwani Kata ya Ilala ambapo wataandaa mipango kazi na bajeti itakayokidhi mahitaji na kutatua changamoto zote zilizopo katika Manispaa hiyo ikiwemo ya maji na barabara ambavyo ni vipaumbele vyake vikubwa.

MwanaHalisi

No comments:

Post a Comment