Saturday, January 30, 2016

Chadema wampa siku tatu Rais Magufuli

Katibu Mwenezi Bavicha Taifa, Edward Simbeyi

BARAZA la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kwa kushirikiana na Umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu Chadema (Chaso) wametoa siku tatu kwa Rais John Magufuli kufuta agizo la Shirika la utangazaji la Tanzania (TBC) kutokurusha moja kwa moja mikutano ya Bunge inayoendelea Dodoma. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mwenezi Taifa Bavicha Edward Simbeyi amesema, kitendo kilichofanywa na Serikali ni udikteta na kwamba, inawanyima wananchi kupata haki yao ya msingi.

“Tunajiuliza maswali mengi, ni vitu gani wanataka kuficha? Hadi wananchi wasivijue? Wakati Bunge linatakiwa kuwa masaa matano na dakika 45 sasa kwanini wanataka kurusha ndani ya saa moja? Haya masaa manne yanaenda wapi? Amehoji Simbeyi.

Amesema hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika ibara yake ya 18 inatoa uhuru wa kila raia kupata au kupewa habari bila ya mashariti kama haya tunayoletewa leo.

“Wanaiogopa mijala inayoendelea Bungeni, Serikali yoyote inayoogopa kukosolewa lazima iyakuwa na mapungufu yake tunacho hitaji ni mikutano uoneshwe live kila mtu ajue kinachoendelea” amesema Simbeyi.

Mbali na hilo, wameitaka serikali kutotumia ubabe ndani ya Bunge kwa lengo la kutaka kuwadhalilisha wabunge wa upinzani, pia Jeshi la polisi lizingatie maadili katika utendaji wao wa kazi na wasikubaliane na kila wanalotumwa na CCM hata kama linavunja sheria.

Amesema kitendo cha Jeshi la polisi kujiingiza katika masuala ya kisiasa ni kujidhalilisha wao wenyewe na ni hali inayoendelea kuwafanya kupoteza uaminifu wao ndani ya jamii.

No comments:

Post a Comment