Tuesday, January 26, 2016

Lowassa, Maalim Seif wateta mazito Dodoma

Viongozi wa juu wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema, Edward Lowassa na wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, walijifungia mjini hapa jana kujadili mambo mawili mazito.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia Nipashe kutoka vyanzo vyetu vya ndani, viongozi hao walijadili mustakabali mzima kuhusu kutangazwa kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar Machi 20, mwaka huu pamoja na uamuzi wa wabunge wao kugomea Kamati za Bunge.

Aidha, viongozi hao baada ya kufia uamuzi, jana usiku walikuwa na mkutano na wabunge wa Ukawa kuwaeleza uamuzi waliofikia na nini wanachotakiwa kukifanya wakiwa bungeni.

"Ni kweli viongozi wa juu wamejadili mambo makubwa mawili, hatma ya uchaguzi wa Zanzibar na kuhusu Kamati za Bunge zilivyoundwa, subiri kidogo tukitoka katika kikao nitakueleza kila kitu," kilieleza chanzo chetu.

Nipashe
 

No comments:

Post a Comment