Saturday, December 5, 2015

Ndalichako ajitosa Umeya jiji la Dar

DIWANI wa Kata ya Chang’ombe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Benjamini Lazaro Ndalichako amejitosa rasmi katika kinyan’ganyiro cha kuwania Umeya wa Jiji la Dar es Saalam.Anaandika Michael Sarungi … (endelea).


Ndalichako ni diwani wa kwanza kurejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo huku milango ya chama hicho kwa nafasi hiyo ikiwa wazi hadi kesho saa nne.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurudisha fomu Ndalichako amesema, ameamua kujitosa kuwania nafasi hiyo huku akijua chamgamoto mbalimbali sugu zinazolikabili jiji hili.

Amesema kwa sasa hivi Jiji la Dar es Salaam linanakabiliwa na changamoto kama matatizo ya hudumaza kijamii kama magonjwa ya mlipuko, upungufu mkubwa wa vitendea kazi ndani ya shule zilizopo ndani ya jiji msongamana wa magari na matatizo mengine mengi yanayohitaji mtu makini kukabiliana nayo.

Amesema yeye kama kijana mwenye sifa kuweza kufanikisha malengo, atahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wa jijiji hili na vyama vyote vya siasa kwa lengo la kuhakikisha jiji linakuwa katika ramani moja na majiji mengine duniani pia kuhakikisha rasilimali zote ndani ya jiji zinatumika kwa manufaa ya wote.

“Tunahitaji kubadilika kwa namna yoyote, hii ni pamoja na kuhakikisha tunabadilisha umangi meza uliozoeleka miongoni mwa watumishi wa jiji hili,” amesema Ndalichako

Amesema endapo atafanikiwa kupata nafasi hiyo atahakikisha anatengeneza ajira kwa vijana wengi kwa kuwajengea uwezo wa kuweza kukopesheka katika benki zilizopo ndani ya jiji hili ikiwemo Benki ya Wananchi (DCB).

Amesema endapo atafanikiwa kupata nafasi hiyo, atakuwa tayari kushirikiana na vyama vyote bila ya kujali itikadi ya vyama.

“Ninawaomba wenzangu wote waniunge mkono katika hili ili tuligeuze jiji letu kuwa katika ubora wa kimataifa na kuweza kutoka hapa tulipo,” amesema Ndalichako

Kuhusu usafi amesema kwa muda mrefu jiji hili limekuwa likinyemelewa na magonjwa ya milipuko kitu ambacho kimesababisha athari kwa maisha ya wananchi wengi.

Na kwamba, hali ilivyo kwa sasa, jiji linahitaji kuwa na kiongozi mwenye upeo wa hali ya juu na mwenye upeo wa kujenga mawasiliano ulio mwema na majiji mengine duniani.

Mratibu wa Kanda ya Pwani, Casmiri Mabina amesema kwa ujumla zoezi linaendelea vizuri na mpaka hivi sasa idadi ya waliojitokeza ni watu wawili ambao tayari wameshachukua fomu na kuomba nafasi hiyo.

MwanaHalisiOnline

No comments:

Post a Comment