Friday, October 2, 2015

MSIFANYE MAKOSA MPENI KUBENEA UBUNGE TUANZE SAFARI - LOWASSA

Hatimaye Mwanahabari Maarufu wa Habari za Uchunguzi Bwana SAID KUBENEA ametambulishwa rasmi na mgombea urais wa UKAWA EDWARD LOWASA katika jimbo la ubungo huku wana ubungio wakiombwa kutokufanya makosa kwa kuhakikisha kuwa wanamchagua mkongwe huyo wa habari kuwawakilisha bungeni.

Akimtambulisha mgombea huyo LOWASA amesema kuwa kwa miaka yote ya ufanyaji wake wa kazi amekuwa akimtambua sana SAID KUBENEA kupitia kazi zake za uchimbuaji wa Habari na sasa anaamini kuwa anafaa kuwawakilisha wananchi wa Jimbo hilo bungeni.

SAID KUBENEA akizungumza na wapiga kura wake amesema kuwa anamini anauwezo mkubwa wa kuwaongoza wananchi wa jimbo hilo kuliko mpinzanzi wake kutoka cha a cha mapinduzi kwa kuwa amekuwa na uzoefu wa kuandika habari za bunge kwa zaidi ya miaka kumi sasa na hivyo hakuna kanuni wala jambo linaloweza kumshinda huku akiahidi kuwa siku atakayoapishwa pale bungeni kesho yake ataanza makeke yake ndani ya bunge hilo.

Kero kubwa ambayo inalikumba jimbo la ubungo ni kerto ya maji ambayo imetajwa kumshinda mbunge anayemaliza muda wake JOHN MNYIKA jambo ambalo Kubenea amesema kuwa MNYIKA amefanya kazi nzuri kulifanyia kazi jambo hilo na sasa kazi iliyobaki ni yeye kuendeleza harakati zake kuhakikisha kuwa kero hiyo inamalizika mara moja.
No comments:

Post a Comment