Tuesday, September 29, 2015

MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA APATA MAPOKEZI MAKUBWA BUMBULI MKOANI TANGA






Mh Edward Lowassa akihutubia mamia ya wakazi wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga.



Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kisiwan, Mji wa Soni katika Jimbo Bumbuli, Mkoani Tanga leo Septemba 28, 2015.


Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la Bumbuli, wakimlaki kwa shangwe Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Kisiwani, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo leo Septemba 28, 2015.


Umati wa Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la Bumbuli, wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kisiwani, leo Septemba 28, 2015.

No comments:

Post a Comment