Wednesday, September 9, 2015

LOWASSA ATIKISA KIBAMBA DAR

Mgombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyama vinavyounda UKAWA, Mh. Edward Lowassa, leo tena amelitikisa jiji la Dar es Salaam, hususan maeneo ya Kibamba kulikofanyika mkutano wa kihistoria wa kampeni ambapo maefu ya wananchi walifurika wengine wakikaa juu ya mapaa ya nyumba za madarasa, wengine kwenye miti, kutokana na kukosa eneo zuri la kuweza kushuhudia "live" mkutanonukiendelea. Changamoto ya maeneo ya kufanyia mikutano ya kampeni ndiyo inayoonekana kuikumba UKAWA, kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaohudhuria mikutano hiyo. Pichani mfuasi wa UKAWA, akiwa amejichora rangi za bendera ya CHADEMA akiambatanisha maneno maarufu yanayotumiwa na wafuasi wa Mh. Lowassa kwa sasa, yaani "Ulipo tupo". 

Mheshimiwa Edward Lowassa akihutubia  katika mkutano mkubwa uliofanyika Kibamba Dar es salaam.


Mh Edward Lowassa akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Kibamba ambaye pia ni Naibu katibu mkuu wa Chadema Bara Mh John Mnyika katika mkutano uliofanyika jimboni Kibamba.Picha zote na Othman Michuzi

No comments:

Post a Comment