Sunday, August 2, 2015

MYIKA AIBUKIA KAMATI KUU

MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika, ameibuka jijini Dar es Salaam na kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu (CC) ya chama chake.
Taarifa kutoka ndani ya kikao cha CC kinachofanyika katika hoteli ya Bahari Beach zinasema, Mnyika amehudhuria mkutano huo na kueleza kuwa kutoonekana kwake, kumetokana na matatizo ya familia.
Mnyika ambaye ni naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amekuwa haonekani tangu Edward Lowassa alipojiunga na chama chake, Jumapili iliyopita.
Mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amethibitisha Mnyika kuhudhuria mkutano huo.
Amesema, “…Mnyika yupo ndani ya ukumbi wa mkutano. Anashiriki kikao cha kamati kuu. Waliokuwa wanadhani chama chetu kimepata mpasuko kutokana na ujio wa Lowassa, walikuwa wanajidanganya.”
Lissu amesema, ndani ya Chadema wako wamoja, yote yaliyotokea yalikuwa mapambano yanayotokana na ukomavu wa kidemokrasia uliyopo.

No comments:

Post a Comment