Friday, August 7, 2015

MTANGAZAJI WA RADIO FREE AFRICA APITA KURA ZA MAONI UDIWANI SASA KUSUBIRI KURA ZA UBUNGE.

SHINYANGA
Mwandishi wa habari na mtangaaji wa Radio Free Africa William Bundala (KIJUKUU CHA BIBI K) ameshinda kura za maoni katika nafasi ya Udiwani katika kata ya Ulowa jimbo la Ushetu.

Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi huo Sangoma amesema kuwa Bundala ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 46 dhidi ya Wagombea wenzake Charles Bahati aliyepata kura 14 na Marco Matheo ambaye hakupata kura yoyote katika kinyang’anyiro hicho.

Kuelekea uchaguzi mkuu Bundala alitangaza nia ya Kugombea Ubunge katika jimbo la Ushetu na udiwani katika kata ya Ulowa huku akisimamia kauli mbiu yake kuwa “Tunahitaji mawazo na nguvu mpya za vijana kuleta mabadiriko ya maendeleo”.

Akiongea kwa njia ya simu akiwa jimboni Bundala amesema kuwa huu ni mwanzo na kuongeza kuwa kwa sasa anasubiri kura za maoni za ubunge ili kuchaguliwa kupeperusha bendera ya Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Sambamba na hayo Bundala amesema kuwa Tanzania ilipofikia kwa sasa inahitaji viongozi wazalendo wenye uchungu na rasilimali za wananchi na siyo kiongozi mwenye uchu wa madaraka anayetaka uongozi kwa rushwa.

Kwa upande wao wagombea waliokuwa katika kinyang’anyiro hicho cha udiwani wamesema kuwa wameridhika na matokeo na kwamba lengo la CHADEMA ni moja kuleta mabadiriko katika jimbo la Ushetu na kata ya ulowa kwa Ujumla.

Kwa sasa Bundala anasubiri kura za maoni za Ubunge zinazotarajiwa kufanyika wiki ijayo huku akiwa katika kinyang’anyiro hicho na watia nia wengine wawili ambao ni Mabula Nkwabi na John Kitibu ambaye alipata kura 45 katika kura za maoni za jimbo la Kahama Mjini katika uchaguzi ambao James Lembeli aliibuka mshindi.

1 comment:

  1. Hongera na tuko pamoja. Mboga wa Chadema hebu jitahidini kutupatia habari za kila siku ndani ya hii upashanaji sio tunazisoma kwingineko. Pia tujizeni loni mgombea wetu ataenda kudaka fomu yake NEC. PIA Kuweni makini sana na magoli ya mkono wanajiandaa kujaza kura walozokwishajipangia. Msikubali. Tusonge mbele. Tumechokaahh.

    ReplyDelete