Sunday, July 5, 2015

‘UKAWA tumejipanga kuipeleka nchi pazuri’

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamejipanga kuitoa nchi kwenye umaskini uliokithiri uliosababisha na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakichukua dola.

Aidha, wamewataka wazee kusimamia kidete kuwasaidia vijana katika zoezi la uandikishaji kupitia mfumo wa kielektroniki (BVR) kwa kuwa wizi wa kura unaanzia hapo na kuwataka wananchi kuhakikisha wanajiandikisha.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam leo na Katibu Mkuu wa Chadema Dk.Wilbroad Slaa wakati akihutubia Baraza la wazee kujadili mustabali ya taifa kuelekea uchaguzi mkuu.

Amesema wazee ndio chimbuko la nchi wanapaswa kusikilizwa na kupewa kipaumbele na kusema kuwa kinachotokea bungeni sasa ni vita kati ya ubadhirifu na ufisadi ndio maana hata wa upinzani wametimuliwa bungeni huku Spika Anna Makinda akitengua kanuni kwa makusudi ili kukilinda chama tawala.

Amesema katika ufisadi chama hicho kinawatumia wazee kuwatoa kutoka mikoa mbalimbali na kuwalipa posho ya shilingi 5,000 ili wahudhurie kwa wingi katika mikutano yao hawana mada za kujenga wanazo za kusambaratisha wananchi.

“Chadema haina uwezo wa kumlipa kila mmoja anayehudhuria katika vikao tuna uwezo wa kuwakusanya na kuwalisha vitu vizuri vya kujenga nchi na si kubomoa”amesemaDk.Slaa.

Akizungumzia baada ya kuchukua dola kupitia UKAWA wataleta mabadiliko katika nchi kwa kuboresha miundombinu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha nyumba za nyasi zinaondoka nchini kwa kuwa Tanzania ina rasilimali za kutosha.

Amesema serikali kupitia CCM wamekuwa wakijisifu kuwa wamewaletea maendeleo wananchi ilihali kuwa maendeleo hayo yameletwa nawananchi wenyewe kupitia kodi zao.

Kupitia mkutano huo Dk.Slaa alivishwa kanzu,koti huku akikabidhiwa shoka kama Chifu wa wazee mkoa wa Dar es Salaam na kubatizwa jina la kizaramo la Mwinyikambi.

Mwanahalisi Online

No comments:

Post a Comment