Tuesday, July 28, 2015

LOWASSA AKARIBISHWA RASMI UKAWA


Waziri mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Ndugu Edward Lowassa leo amekaribishwa rasmi kujiunga na Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA). Akiongea mbele ya waandishi wa Habari kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Wananchi (CUF) Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mh James Mbatia amesema ‘tumemkaribisha Mh Lowassa kujiunga na UKAWA ili kuongeza nguvu ya kuhakikisha tunaitoa CCM madarakani kwani tunaamini Mh Lowassa ana uwezo wa kuhamasisha umma kuitoa CCM Madarakani katika uchaguzi mkuu ujao’. Mkutano huo umehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Lipumba na Mwenyekiti wa NLD Mh Emmanuel Makaidi.

Pichani kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mh James Mbatia na Mwenyekiti wa NLD Mh Emmanuel Makaidi walipokuwa katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika Makao makuu ya chama cha Wananchi CUF, Buguruni Dar es Salaam.
Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA wakinyanyua juu mikono kama ishara ya mshikamano katika kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

2 comments:

  1. Mungu ni Mwema tumeishi kuziona siku hizi za Neema, baba zetu mama zetu na ndugu zetu walitamani kuziona siku hizi CCM ikifa lakini hawakuziona. Mungu ashukuriwe

    ReplyDelete
  2. Namshukuru Mungu tumeishi na kuziona Nyakati hizi ambazo watu wengi walitamani kuziona lakini hawakuona, Mungu ni mwema mwisho wa CCM umefika

    ReplyDelete