Wednesday, July 29, 2015

LOWASSA AJIVUA GAMBA NA KUVAA GWANDA

Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa leo amejiunga na UKAWA kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika hafla iliyohudhuriwa na waandishi wa Vyombo Mbalimbali vya habari. Hafla hiyo ambayo imehudhuriwa na Viongozi wote wanaunda umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA akiwemo mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR Maeuzi Mh James Mbatia na Mwenyekiti wa NLD Mh Emmanuel Makaidi.
Lowassa ambaye aliambatana na mkewe Mama Regina Lowassa wote walikabidhiwa kadi ya kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema na Mh Freeman Mbowe.
Katika Hotuba yake mara baada ya kutangaza kujiunga na Chadema Mh Lowassa ameongelea mambo mengi yaliyomshawishi kujiondoa CCM na kujiunga na UKAWA kupitia CHADEMA hosusani suala la mchakato wa kupata Mgombea Urais kupitia CCM lilivyotawaliwa na zengwe. Katika Hotuba yake Mh Lowassa amewaomba Watanzania wote wenye kulitakia mema Taifa Kujiunga na UKAWA kwa ajili ya kutimiza Safari ya Matumaini.

Pichani kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mh James Mbatia, Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe, Waziri mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa na Mwenyekiti wa CUF Prf Ibrahimu Lipumba.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya kujiunga na CHADEMA Waziri mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa.

Mh Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya Kujiunga na CHADEMA mama Regina Lowassa.

Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa na Mkewe mama Regina Lowassa wakionyesha kadi zao za Uanachama wa CHADEAMA mara baada ya kujiunga na CHADEMA katika hafla iliyofanyika Bahari Beach Hotel.
Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa akiwa na Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Lipumba

Mwenyekiti wa Baraza la wanawake CHADEMA na Mbunge wa Kawe Mh Halima Mdee akisikiliza kwa makini yaliyokuwa yakijili katika hafla ya kujiunga na Chadema kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh Edward Lowassa.

No comments:

Post a Comment