Benson Kigaila, Mkurugenzi wa Oganaizeisheni na Mafunzo ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),imeibuka kidedea katika kura za maoni kuomba ridhaa kugombea ubunge Jimbo la Dodoma Mjini.
Kigaila amewabwaga kwa mbali wapinzani wake wanne ambao nao waliomba ridhaa ya kuchaguliwa katika kura za maoni ili kuweza kupeperusha bendera ya Chadema katika kusaka ubunge katika jimbo hilo.
Pamoja na ushindi wa Kigaila, kada wa chama hicho, Josephine Kihoza ambaye alitangaza nia ya kuomba ridhaa ya kupitishwa katika kura za maoni ili awanie jimbo hilo naye alichomoza kwa kuwa mshindi wa pili huku akiwabwaga wenzake kwa mbali zaidi.
Katika kura za maoni Kigaila alipata kura 168 huku mpinzania wake Joseph Kihoza akiwa na kura 25 na aliyefuatia alikuwa na kura 4 na wengine waliwa wakifungana kuwa na kura tatu tatu.
Awali katika Mkutano mkuu maalum wa uchaguzi ulifanyika mjini hapa huku ukiwa chini ya usimamizi wa mwenyekiti wa muda wa uchaguzi mzee, Eneck Mhembano ambaye aliwahi kupepeprusha bendera ya Chadema kwa kuwania nafasi ya ubunge mwaka 2010 na kuibuka mshindi wa pili wali aliwataka makamanda wa Chadema kuhakikisha wanashirikiana katika kufanya kazi za chama na kukijenga chama hicho.
Amesema wakati yeye akigombea ubunge hapakuwa na wapinzania ndani ya chama kwa maana ya kupiga kura za maoni kama ilivyo sasa.
“Mimi wakati nagombea hayakuwepo haya yote ya kura za maoni bali walikuja wakaniomba nigombee na wakanipa katiba ya Chadema nikaisoma vizuri na nikaielewa nikaingia ulingoni na nilipata kura nyingi nikawa waili dhidi ya mgombea wa CCM.
“Lakini angalia kwa sasa chama kinakua hadi tunafanya kura za maoni ili kumpata mgombea mmoja sasa na sema ni lazima apatikane mmoja na hakuna mshindi hapa wa mshindi ni chadema wala siyo mtu.” Amesema Mbembano.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mkoa wa Dodoma Jella Mambo amesema kwa sasa chama kina kazi kubwa moja ya kuiondoa CCM madarakani kutokana na kushindwa kuwapatia maendeleo wananchi.
Mbali na kushindwa kuwapatia wananchi maendeleo CCM imekuwa ilikumbatia wizi, ufisadi na masuala ya Rushwa huku watanzania wengi wakiendelea kuwa masikini.
Kigaila wakati akitoa shukrani kwa wapiga kura alisema kazi kubwa ni kuhakikisha anaambana na ufisadi na manyanyaso ambayo wanafanyiwa wakazi wa Dodoma hususani katika masuala ya ardhi.
Mwanahalisi Online
No comments:
Post a Comment