Sunday, July 19, 2015

John Heche Kugombea Ubunge Tarime Vijijini kupitia Chadema


John Heche aliyekuwa mwenyekiti wa vijana Taifa Chadema (Bavicha) ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge jimbo la Tarime vijijini. Mwanzoni John Heche alikuwa ametangaza nia kugombea ubunge Tarime Mjini. Isipokuwa  kwa busara pamoja na mapenzi mema ya Chadema ameamua kugombea vijijini ili makamanda wengine waweze kuendelea na harakati TarimeMjini. Kwa ujumla Tarime Vijijini ina kata 28. Wakazi wa tarime wamefurahia sana kwa maamuzi mazuri aliyofanya kamanda John na wameahidi kufanya naye Kazi kipindi kampeni zitakapo anza mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment