Friday, July 31, 2015

JAMES LEMBELI ASHINDA KURA ZA MAONI UBUNGE KAHAMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wilayani Kahama mkoani Shinyanga jana kimemtangaza Ndugu Daudi James Lembeli kuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama kupitia chama hicho katika uchaguzi uliofanyika mjini Kahama.
Akitangaza matokeo hayo mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya wa chama hicho Msimamizi wa uchaguzi King Haile amesema kuwa idadi ya kura zilizopigwa ni 262 zilizotarijiwa kupigwa ni 292 na kwamba kura zilizoharibika ni kura 3.

Katika uchaguzi huo Mh Lembeli amepata ushindi wa kura 168 akifuatiwa na John Kitibu aliyepata kura 45,huku Anord Nshibo akipata kura 17 na Emmanuel Madoshi akipata kura 10.

Wengine ni Felician Maige na Joseph Nyerere waliopata kura 4,Zacharia Obed amepata kura 3 huku Prosper Ndege,Anord Ernest na Thadeo Mwati wakipata kura 2.

Sambamba na hao Ruben Lucas na Deusdediti Mabinda wamepata kura 1 nao Richard Martin na Victor Bwana wakipata sifuri katika uchaguzi huo.

Kwa upande wa ubunge wa viti maalumu aliyeshinda ni Winfrida Mwinula aliyepata kura 34,akifuatiwa na Salome Mapamba aliyepata kura 30 huku Merry Sumuni akipata kura 9 na Magreth Mlekwa akipata kura 4.

Wakiongea baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo wagombea ambao kura zao hazikutosha wamesema kuwa Ushindi wa James Lembeli na Winifrida Mwinula ni ushindi wa chama hivyo wanaungana nao katika kuhakikisha wanapata ushindi wa Kishindo katika uchaguzi mkuu ujao.

Akitoa shukrani mara baada ya kutangazwa mshindi Mh Lembeli amesema kuwa ushindi huo ni salamu kwa Chama cha mapinduzi kuwa ni dalili za kushinda katika majimbo yote ya Kahama mjini,Ushetu na Msalala.

No comments:

Post a Comment