Katibu Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibroad Slaa akiwa na Mshauri wa
Masuala ya Uchumi, Sayansi na Maendeleo ya Jamii katika ulimwengu wa dijiti
(digital), Dk. Mario Voigt, walipokutana Villa La Collina, Milan kwa ajili ya kujadiliana
na kubadilishana uzoefu kuhusu namna bora ya kusimamia uchumi unaonufaisha
wananchi hususan kwenye nchi zenye utajiri wa rasilimali lakini watu wake
wanakabiliwa na umaskini, kama Tanzania. Dk. Voigt ni mtaalam katika eneo hilo,
akitokea iliyokuwa Ujerumani Mashariki, ambayo uchumi wake ulikuwa ukiendeshwa
na sera za kisoshalisti kabla ya kupitia mabadiliko makubwa kutoka hali duni na
sasa sehemu hiyo ni mojawapo ya jamii zenye maendeleo makubwa ndani ya
Ujerumani. Dk. Slaa yuko ziara ya kikazi barani Ulaya kwa siku 7. (Na mpiga
picha maalum).
No comments:
Post a Comment