Saturday, May 23, 2015

Viongozi wakuu CHADEMA kutikisa nchi leo na kesho


Tunapenda kuwatangazia wananchi kote nchini hasa katika mikoa ya Dar, Bukoba, Mbeya, Tabora, Simiyu na Mwanza, ambako viongozi wakuu wa chama watakuwa na majukumu mbalimbali...

DAR ES SALAAM;

Leo Jumamosi Land Mark Hotel, Ubungo Wakili Mabere Marando, Prof. Baregu na Mbunge wa Ubungo Mnyika watahudhuria na kutoa mada kwenye kongamano la mahafadhali ya vijana wa CHASO wanaotarajia kuhitimu vyuo hivi karibuni. Kongamano litaanza saa 4.00 asubuhi.

KAGERA;

Katibu Mkuu Dr. Slaa anaanza ziara ya siku 3 mkoani humo ambapo leo atakuwa na mkutano wa hadhara mjini Bukoba, kisha Jumapili atakuwa Karagwe na Jumatatu atakuwa Muleba.

Mbeya Mjini;

Baada ya ziara iliyomfikisha juzi Rungwe na jana alikuwa Kyela, Mwenyekiti wa Chama Taifa leo atakuwa Mbeya mjini ambapo atakagua zoezi la uandikishaji wapiga kira katika vituo mbalimbali ili kujionea hali halisi inavyokwenda.

TABORA;

Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara, Prof. Abdallah Safari atakuwa mjini Tabora siku ya Jumapili ambapo atafanya mkutano wa hadhara baada ya kuhudhuria mahafali ya CHASO Kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali mjini humo.

Mwanza na Simiyu

Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu leo Jumamosi atakuwa mgeni rasmi katika mahafali ya wanafunzi wa CHASO Chuo Kikuu cha SAUT, kisha atafanya mkutano wa hadhara mjini Magu na baadae jioni atakuwa na kikao cha ndani Mwanza Mjini.

Siku ya Jumapili atafanya mkutano wa hadhara mkoani Simiyu kabla ya kuelekea wilayani Sengerema Kwa ajili ya kongamano la mafunzo ya vijana wa CHADEMA kuhusu uzalendo Kwa nchi yao.

TAIFA KUZIZIMA KESHO

Kesho Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe atatetemesha nchi kwa kuzungumza na Taifa kupitia mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe DSM.Mkutano huo utarushwa moja kwa moja na ITV

Tunaomba wananchi na wafuasi wetu kote nchini waendelee kuunga mkono chama chao.


Tumaini Makene

MKUU WA IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO-CHADEMA

No comments:

Post a Comment