Wednesday, May 27, 2015

Chadema yawaonya Viongozi wa Dini Mamluki.

Na. Bryceson Mathias, Mvomero Morogoro
WANACHAMA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Mvomero, wamewaonya Viongozi wa Dini waliotia Nia ya Kugombea Uongozi katika Chama chao, wasithubutu kuwa Mamluki, maana watawashitaki kwa Mungu, na wakiendelea kwa Shetani.

Akihojiwa na Mwandishi juu ya kuwepo kwa tuhuma za Viongozi hao wanaodaiwa kujipenyeza ndani ya Chadema kama Mamluki, Katibu wa Chadema Mvomero, Ramadhani Mrisho, amewaonya viongozi hao kama wapo, maana hakuna Mharifu yeyote atakayepenya.

Hatua ya Wanachama wa Chadema Mvomero kuonya Viongozi hao, imefuatia kuwepo kwa fununu za watia nia hao kutumia fedha jimboni humo, ambapo walidai wanaunga Mkono Kauli ya Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, ambaye hivi karibuni Mbeya, aliwaonya Wagombea wa Chadema, asiwepo atakayethubutu Kutumia Fedha kujipatia Uongozi.

Mrisho alikiri; Anao Viongozi wa Dini zaidi ya wanne toka madhehebu mbalimbali waliotia nia ya kugombea Uongozi tangu ngazi ya Msingi hadi Ubunge, huku akikiri na kusema kwa kutumia uwezo wao wameweza kukifikisha Chama hadi Ngazi ya Msingi;

“Hata mimi nimesikia minong’ono ya nje ya Chama kuhusu baadhi ya Viongozi hao kudaiwa wanatumia nguvu ya fedha kusaka uongozi huo; Lakini nataka nionye!! Kama atatokea mwenye nia Ovu ya kukihujumu Chama kwa njia hiyo: Hatoki Ng’o, tutakula naye sahani Moja”!!.

Aidha alidai, “Nina Imani kubwa na Kamati Kuu ya Chadema Taifa, kwenye kura ya Maoni na Uteuzi wa wagombea, kwamba itafanya Kazi Nzuri na ya Haki, kutokana na jinsi ilivyo makini, maana, taarifa zote inazo kabla ya Jogoo halijawika. Hivyo nina Uhakika, kama Mharifu yupo, Hapenyi Ng’o!!, Labda Kamati iwe imeacha wajibu wake”. alisema Mrisho.

Mapema katika Mchakato wa kuwania Ubunge katika Majimbo yanayoshikiliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), yanayowindwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamejitokeza baadhi ya Viongozi wa Dini na Watia Nia Mamluki, wanaodaiwa kutumika kuudhoofisha Umoja huo kwa nafasi hizo, ili kuwakwamisha UKAWA.

No comments:

Post a Comment