Thursday, April 2, 2015

Waziri amtenga Diwani wa Chadema asimuone Pinda.

Na Bryceson Mathias, Morogoro.
NAIBU Waziri wa Maji na Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amosi Makala, amemtenga Diwani wa Kata ya Mtibwa, Luka Mwakambaya (Chadema), katika safari ya Wafanyakazi na Wakulima waliokwenda kumlalamikia Waziri Mkuu Mizengo Pinda, juu ya Ukatili wa Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa.

Akizungumza na Tanzania Daima, Mwakambaya alisema, Safari ya kwenda kumshitaki Mwekezaji huyo ilikuja baada ya Wafanyakazi na Wakulima wa Miwa ya nje kukasirishwa na na Ukatili wa kutowalipa Mishahara na Malipo ya Miwa waliyomuzia kwa miezi zaidi ya Mitatu.

Amesema, Hasira ya Wafanyakazi ilipanda zaidi pale ambapo, Machi 22, mwaka huu, Mwekezaji alitoa Sekula Na. C.1/18/2015 ya 22/3/2015 iliyonakiliwa kwa Wakuu wa Idara, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Tawi la Mtibwa (TPAWU) na Mbao zote za Matangazo.

Tangazo hilo Maalum kwa Wafanyakazi wote Mtibwa Sugar Estate (MSE Ltd), lilikuwa na maagizo matano ya kuwanyanyasa, kuwatisha, kuwagandamiza na kuhodhi haki za msingi za Sheria za Kazi, akitaka Wafanye kazi kwa mishahara ya kuchelewa, au waombe likizo bila Malipo, na asiyefanya kati ya hayo hataingia kazini na atakuwa amejifukuzisha kazi.

“Namshangaa Naibu Waziri ambaye tunajenga nyumba moja ya kuwahudumia Wananchi, amenitenga kwenda kwa Pinda akijua kuwa maelezo nitakayompa yatakuwa hayana Chenga juu ya Ukatili wa Mwekezaji huyo, na badala yake ameamua kufanya siasa za kugombea Fito.

Mara kadhaa amekuwa hayupo jimboni na kwenye Kata, lakini mimi ndiye ninayekabiliana na adha ya huyo mwekezaji kwa wananchi, kiasi cha kumlazimisha mwekezaji huyo kulipa miezi kadhaa kwa kupiga kambi mlangoni kwake, lakini leo anafanya ndoto za alinacha”.alisema Mwakambaya.

Alisema, katika Msafara huo wa Kisiasa, wamo Mwenyekiti wa Chama wa Wafanyakazi wa Mashambani na Kilimo (TPAWU), Katibu wake, Wenyekiti wawili wa Chama cha Wakulima wa Miwa ya Nje (MOA na TUCCOPRICOS, Katibu wa Mbunge Makala, na Katibu Mwenezi wa CCM (W).

Mwakambaya ameuomba Uongozi wa Chadema Taifa, kumsaidia kunyausha Uongo wa kisiasa unaofanywa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwahadaa wananchi hao huku kikikumbatia Ukatili wa Mwekezaji wa Kiwanda hicho kuwadhulumu Wafanyakazi na Wakulima na kumlinda Kada anayemiliki kiwanda hicho.

Aidha Tanzania Daima, limefanikiwa kuona Sekula hiyo Na. C.1/18/2015 ya 22/3/2015 ilitiwa Sain na Kaimu Meneja Rasilimali Watu, VT Mazengo, na Meneja Mkuu wa Kiwanda, Hamad Yahya, ambapo maagizo yaliyomo humo, hayamo hata kwenye Sheria za Kazi dunia kote, isipokuwa kwa Mwekkezaji huyo wa Tanzania inayojiita ina Serikali Sikivu.


No comments:

Post a Comment