Thursday, April 30, 2015

NGUZO 5 IMARA ZA CHADEMA

Tunapoelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu (2015), tunaingia na chama kikuu, imara, makini kuliko muda wowote katika historia ya nchi hii. Sababu za chama hiki kuingia kikiwa na nguvu kiasi hiki ni tano na unaweza kuziita nguzo za chama.

1. Mwenyekiti na Katibu mkuu
Mtakumbuka kabla ya uchaguzi wa ndani wa chama kulikuwa na juhudi za kuwagombanisha toka kwa mahasimu wetu (walio ndani tunajua mengi) Mbinu hiyo iliposhindikana wakaja na mbinu ya kuwazuia kugombea, wakatumia ofisi ya msajiri na kelele za vyombo vyao vya habari. Kama kawida yao viongozi wetu walitulia na kuendeleza mpango wa uchaguzi na mkutano mkuu uliofana na ambao haukuwahi kufanyika na chama chochote katika ardhi ya Tanzania. Ushirikano wao na mealewano yao ni nguzo kuu ya chama.

2. Idara ya usalama ya chama:
Kwa yoyote anayejua hujuma za siasa za Tanzania atashangaa ni kwa jinsi gani chama hiki kimeweza kukwepa mishale ya ndani ya chama na nje ya chama. Ccm wametumia kila njia kuiua Chadema, kuanzia kupandikiza mamluki, kudhuru vingozi wakuu, kufanya kila njama kuona chama kinakufa. Wakati wote idara hii mahiri imenasa mipango yao yote, pamoja taarifa za idara kukiokoa chama na viongozi lakini pia wakati mwingine hutumika kama kete za kisiasa. (hapa kuna njama nyingi, ugaidi wa Rwakatale, SMS za Mwigulu, Mauaji ya Soweto, njama za kumdhuru Dr Slaa kwenye helkopita, Khalid Kagenzi, mpango wa mapinduzi ya uongozi wa chama nk nk nk.)

3.Wanasheria wa chama:
Mahasimu wetu wamejitahidi kuwabambikiza kesi vingozi, kuzia baadhi ya harakati zetu kisheria, kutengua wabunge wetu, kuhoji baadhi ya maamzi ya chama mahakani. Kinara wa sheria nchini Tundu Lissu na timu yake kama kina Prof Safari, Mabere Marando, Kibatala, Kimomogoro, Mbogolo, Mdee mara zote wameubuka washindi katika kesi hizi. Ukienda vyuo vikuu vingi wanavyuo wanasoma sheria kwa sasa role model wao ni wanasheria hawa na hasa Tundu Lissu.

4. Timu ya mipango:
Kama kuna kitu kinawasumbua mahasimu wetu ni jinsi mipango ya chama inavyokuwa ya kisasa, inayokwenda na wakati na isyotabilika. Wakiwa wanajipaga kuhujumu mpango unaendelea uantokea mpango mwingine wa hali ya juu, maadui wetu hulazimika kurudi kwenye drawing board kujipanga upya. M4C, mpango wa kanda, Chadema ni msingi, FTP 200, na sasa timu za kampeini ni baadhi ya mipango hiyo. Wakati wanajipanga kuhujumu FTP 200, sisi tuko mbele yao maana tumeanza timu za kampeini.

5. CHASO
Hii ni jumuhiya ya wanafuzi wanachadema vyuo vikuu, hawa kwa asilimia kubwa ndiyo wagombea nafasi mbali mbali mwaka huu, wameiva kifalsafa na kiitikadi. Wamenieneza Chadema kwa nguvu zao zote, si waoga na sasa wameanza mpango wa kusambaa nchi nzima kueneza Chadema kitaaluma. Siku moja Shonza aliwahi kuhoji humu eti CHASO ya akina ZZK na Regia (R I P) Mtema iko wapi. Alishindwa kujua hawa ndiyo watumishi wa leo wako ofisini na kadi za Chadema mifukoni! Ameshindwa kujua ndiyo wanaotangaza nia ya kugombea ubunge kiasi kwamba kila jimbo la Tanzania bara lina watia nia zaidi ya watano.

No comments:

Post a Comment