DIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Mtibwa wilaya ya Mvomero, Luka Mwakambaya, amembana kwenye Kona na kumyima Usingizi Naibu Waziri wa Maji na Mbune wa Jimbo hilo, Amosi Makala, kiasi cha kumfanya ahofie Ubunge wake 2015 na kuamua kumshitakia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda; Chadema wakidai hilo ni change la Macho.
Hofu ya Makala inatokana na Kijiji na Serikali ya Mji Mdogo wa Madizini anaokaa, kunyakuliwa na Chadema wakiwemo Viongozi wenzake wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri Mvomero, Mwenyekiti wa CCM na Katibu Mwenezi, kuongozwa na Chadema.
Makala akiwa bungeni hivi karibuni alimlalamikia Pinda hatari ya kupoteza jimbo hilo kwa upinzani, pale alipofanikiwa kuwakokota Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi Mashambani na Kilimo Tanzania (TPAWU), Wakulima wa Miwa ya nje MOA na TUCCOPRICOS, wanaotofautiana na Mwekzaji waKiwanda cha Sukari Mtibwa, asiyewalipa malipo yao, wakitaka Mwekezaji mpya.
Katika msafara huo ambao Diwani Chadema alitengwa, CCM kiliwapiga Changa la Macho Wafanyakazi na Wakulima hao bila kuwapa majibu kama kitamng’oa mwekezaji huyo kama walivyopendekeza, bali walimkumbatia Mwekezaji huyo, anayedaiwa Mishahara ya Miezi Mitatu na Wafanyakazi, ikidaiwa Wakulima wanadai Bil. 1.270/-, amelipa Mil.150/- tu!.
Habari zilizonaswa toka kwenye Kikao hicho zinadai, licha ya Wakulima na Wafanyakazi kutoa Kero Sugu za Mwekezaji huyo, Pinda alikiri kuzifahamu na kuzisikia mara kadhaa, lakini inadaiwa alisema, hana jibu la haraka, ila anaandaa Kikao na Mawaziri husika wa Viwanda, Kilimo na Mwanasheria Mkuu, ichunguzwe Mikataba yake.
Aidha inadaiwa alisema, ataandaa Ziara Maalum kwenye Viwanda vya Sukari Kilombero, Kagera, TPC na Mtibwa, ili Mawaziri husika na wanasheria Mkuu, Waweze kuona nini kifanyike kama Mikataba hiyo iko fyongo au kiwete inayowaumiza.
Mwenyekiti wa TPAWU Tawai la Mtibwa, Dominick Bayogire Mbasha, alipoulizwa ukweli wa safari yao kwa Pinda alikiri kuwa, Majibu waliyopata hayana Mashiko wamepigwa Changa la Macho na kwamba safri hiyo ilikuwa ya Kisiasa, na kwamba familia zao zitaendelea na shida.
Tuliopigwa Changa la Macho katika Msafara huo si mimi tu ni pamoja na Katibu wa TPAWU Taifa, Mwenyekiti wa TPAWU Mtibwa, Mbasha, Mwenyekiti, Mjumbe wa TPAWU Mtibwa, Waziri Mdemu, Katibu wa Mbunge, Jumanne Kombo, na Wenyeviti wa Wakulima wa Miwa ya nje MOA na TUCCOPRICOS, walitoa Hoja ya kutkaka Mwekezaji mpya haraka kama Wafanyakazi, au kijengwe Kiwanda kingine.
Wakati tunaenda mitamboni, tayari Wakulima wa Nje wa Kiwanda cha Mtibwa, wamefunga Mageti ya Kiwanda cha Mwekezaji, kutokana na ahadi ya kuingiziwa fedha kwenye Akaunti ya Vyama hivyo vya Wakulima, ambapo hata Kampuni ya Usafirishaji Miwa ya KIOMA inadai Mil.440/-, huku wakikasirishwa na taarifa za Safari ya Dodoma.
No comments:
Post a Comment