Saturday, April 4, 2015

Chadema kuzindua Kanda mpya Kusini.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinatarajia kuzindua Kanda mpya ya Kusini itakayoundwa na mikoa miwili ya Lindi na Mtwara.

Akizungumza na NIPASHE juzi, Ofisa wa chama hicho Kanda ya Kusini, Filbert Ngatunga, alisema mwanzo Kanda ya Kusini ilikuwa inaundwa na mikoa mitatu ya Lindi, Mtwara na Ruvuma na makao makuu yake yalikuwa mjini Songea mkoani Ruvuma.

Alisema kutokana na maboresho yaliyofanywa na chama hicho, waliamua Mkoa wa Ruvuma kuuhamishia katika Nyanda za Juu Kusini na hivyo kuungana na mikoa ya Njombe, Mbeya, Iringa na Rukwa na hivyo kanda hiyo kuundwa na mikoa mitano.

Aliongeza kazi hiyo itafanyika Aprili 11 na 12, mwaka huu na kuhudhuriwa na viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika.

Alisema kabla ya uzinduzi huo, kutakuwa na vikao vya ndani na kufuatiwa na mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mashujaa.

No comments:

Post a Comment