Tuesday, April 28, 2015

BARAZA LA VIJANA (BAVICHA) MKOA WA MBEYA

BARAZA LA VIJANA (BAVICHA) MKOA WA MBEYA

Tarifa kwa umma,

Bavicha tunalaani kitendo cha Jeshi la Polisi Mkoani hapa kuwakamata vijana wa Red Brigade wa Tunduma na kuutangazia umma kuwa wamekutwa na silaha za kivita jambo ambalo si kweli.

Ikumbukwe siku ambayo Mathew Mwafongo maarufu kama 'Ras' na Salehe Sichalwe walikamatwa na Polisi katika eneo la Sogea Tunduma wakiwa wanajiandaa kwenda Momba Vijijini ndipo askari hao walimkamata na kuwawekea Visu ndani ya gari waliyokuwa wakitumia. Askari hao waliwapeleka kituo cha polisi Tunduma na wakautangazia umma kuwa watu hao ni magaidi jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote.

Kwa nyakati tofauti kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya RPC Msangi alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akiwahusisha vijana hao na ugaidi,Alsha-bab na jana aliutangazia umma kuwa ni majambazi.

Kauri ya RPC Msangi inalengo la kukichafua Chama na Baraza la Vijana ili jamii ione CHADEMA na viongozi wake hawafai mpango ambao umefeli na katu hautaweza kufanikiwa kuidhoofisha harakati za ukombozi katika Mkoa huu.

Tunalaani kitendo cha Jeshi la Polisi kuendelea kutumika kukihujumu Chama chetu na kuwa kamata na kuwabambikia kesi watu wasio na hatia.

Tunalitaka Jeshi la Polisi kuacha mara moja mchezo wa kukamata vijana wa CHADEMA na kuwapakazia kesi,Bavicha hatutaendelea kuwafumbia macho na badala yake tutachukua hatua zaidi.

Kitendo cha jeshi hilo kuendelea kufanya hivyo ni kujenga chuki miongoni mwa jamii yetu jambo ambalo si zuri sana kwa mustakabari wa taifa letu.

Natoa Rai yangu kwa polisi wote nchini kuwa wafanye kazi kwa weledi huku wakizingatia maadili ya kazi yao na si kutumiwa na Chama tawala katika kukabiri nguvu ya upinzani nchini.

Imetolewa April 27,2015

NA:

GEORGE TITO
MWENYEKITI WA BAVICHA
MKOA WA MBEYA.


No comments:

Post a Comment