Friday, March 6, 2015

M/kiti CCM; amtaka Halima Mdee Chadema awasaidie.

Na Bryceson Mathias, Mandera.

MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Mandera, wilayani Kilosa, Morogoro, Salum Njagila (CCM) amelaani Halmashauri ya Wilaya hiyo, kukumbatia Ardhi iliyobatilishwa Umiliki wake na Serikali, akidai Mafisadi wa Ardhi nchini, wanawahujumu Wakulima,.

Njagila baada ya kuoneshwa barua ya Idara ya Utawala na Ardhi inayayosema Mashamba Na. 33-38, 40 na 40A, yalibatilishwa na Rais Umiliki wake, amemuomba Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee (Chadema), awasaidie.

Njagila alisema hayo, alipohojiwa na Tanzania Daima, iwapo ana taarifa za Ubatilisho wa Milki za Mashamba Na.33-38, 40 na 40A ya Magole Kilosa, ambayo kwa Barua Kumb. KL/MMAG/141 ya Oktoba 31, 2012, waliiomba Serikali iwarejeshee kwa vile hayaendelezwi.

Njagila alishangaa kuiona barua ya Kamishina wa Ardhi nchini Kumb. LD/30305/112 ya Septemba 9, 2013, ambayo Serikali kupitia kwa Rais, Januari 1986, ilifanya Ubatilisho wa Milki za Mashamba hayo kutokana na Wamilikaji kushindwa kutimiza Masharti ya Umilikaji.

Mashamba hayo ambayo yalitakiwa yawe yamegawiwa kwa Wananchi kwa ajili ya Kilimo, bado yaliendelea kumilikiwa kinyume cha Sheria na wahusika, huku mengine yakiwekewa, Rehani na Mikopo ya Dhamana, ili hali wananchi wanakosa pa kulima.

Taarifa za Mashamba hayo zinaonesha, Milki ya Shamba Na. 35 lililomilikiwa na Mrza Alaudin Hati 9047, lilibatilishwa na Rais Januari 14, 1986, ambapo shamba na. 36, linamilikiwa na, Issa Salum, kinyume na taarifa za kumilikiwa na Nyakunga Magairo.

Shamba Na. 38 linamilikiwa na, Sadrudin Kassam, kama dhamana ya Mkopo wa Shilingi 60,000/-, ambapo ulisainiwa chini ya FD Na. 42032; ambapo ubatilisho wa Mashamba Na. 37, 40 a 40A, ulikuwa unaendelea, huku Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, ukitakiwa kutuma Vivuli vya Ilani kwa Wamiliki.
Aidha wakati wananchi, Wakulima na Wafugaji wilayani Kilosa, wakiuana ovyo na kulalamikia ukosefu wa Ardhi na maeneo ya Kilimo na Malisho, bado Wamiliki Uchwara, wameendelea kushikilia, kuhodhi na kumiliki Mashamba ambayo Serikali kupitia Wizara na Rais, ilisha yatolea Ubatilisho wa Matumizi, lakini wanendelea kuyatumia kwa Mlango wa Nyuma.





No comments:

Post a Comment