Monday, March 23, 2015

Chadema, ‘Heri Shetani unamyemjua, Kuliko Malaika usiyemjua’.

Na Bryceson Mathias, Njombe.
DIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kata ya Mtibwa, Luka Mwakambaya, akiwa Njombe Kichama, ametuma Salamu kwa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mvomero kuwa, ni Heri kuwa na Shetani unamjua, kuliko Malaika usiyemjua.

Mwakambaya alisema hayo jana, kufuatia mbinu za CCM alizodai ni Kujikomba, kwa Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa, awalipe Wakulima na Wafanyakazi Mishahara ya Mwezi wa Pili na wa Tatu kwa Mazungumzo kwa vile ni Kada wao, ili kuikejeli Chadema ambayo awali ilikesha na Wafanyakazi nje ya lango la Mwekezaji na Wakalipwa malipo yao!.

Uchunguzi wa Tanzania Daima umebaini, Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amosi Makala, Jumanne Kombo, alifanya Mazungumzo na Meneja wa Kiwanda, Hamad Yahya, awalipe Wadai hao, kama njia ya kuponda hatua za Chadema, lakini akakwama.

Wakiwa wamekata tamaa ya kulipwa, Wafanyakazi na Wakulima wadogo wa Miwa, wanaodai Malipo, kwa nyakati tofauti wamesema, walimshangaa Kombo, kupoteza muda kujinasifu kutafuta umaarufu, kwamba Mwekezaji ni Kada wa CCM, Chadema wakidai, Mwekezaji ni Sikio lisilosikia Dawa.

“Mwekezaji wetu kazoea kulipa Wakulima na Wafanyakazi Malipo hadi atajwe bungeni, afanyiwe Maandamano au afungiwe Milango; Hivyo kwa kuwa amekuwa sugu, Utamaduni wa mazungumzo mezani, kwake ni ndoto za alinacha, hasikii la Shekhe wala la Mchungaji.

“Nawataka Wakulima na Wafanyakazi wanaonyanyasika Wanafunzi kurejeshwa Shule kwa kutolipa Ada kutokana na Mwekezaji kuhodhi Malipo yao; Wajue ni Heri Shetani unayemjua (Maandamano ukapata haki), kuliko, Mazungumzo na Malaika usiyemjua, Usilipwe”.alisema Mwakambaya.

Mwakambaya alimuonya Mwekezaji kuwa, awalipe haki zao Wakulima na Wafanyakazi hao, siku tatu kuanzia sasa kabla hajafika, la sivyo akifika atatumia tena mfumo wa ‘Heri Shetani unamyemjua kuliko Malaika usiyemjua, wa kulala langoni kwake wakisonga Ugali, hadi walipwe’.

Awali Mwekezaji kupitia kwa Meneja wa Kiwanda Hamad, aliahidi kuwalipa Wakulima na Wafanyakazi hao Ijumaa au Jumamosi iliyopita lakini hakuwalipwa, hivyo wanasubiri ‘Msukumo wa Nguvu ya Umma’ utakaopangwa na Chadema, Mwakambaya akiongeza hata kama watapigwa Mabomu na Polisi walioizoe kuitetea CMM na Wawekezaji kwa kuagizwa na Watawala.
Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Luka Mwakambaya, siku alipolala nje ya Lango la Mwekezaji wakishinikiza Malipo ya Wafanyakazi ambapo walilipwa Mwezi mmoja. 


Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa wakiwa nje ya Kiwanda wakishinikiza kulipwa Mishahara yao ya Miezi Mitatu 

No comments:

Post a Comment