Sunday, February 22, 2015

Mkutano wa CHADEMA viwanja vya Dr Slaa - Mbeya

Muda huu mwenyekiti wa chama Taifa anahutubia mkutano kwenye viwanja vya Dr Slaa hapa Mbeya mjini.

Ni mkutano wa hadhara baada ya kumaliza kikao cha ndani cha baraza la uongozi la kanda ya Nyanda za juu Kusini, kanda hii ina mikoa ya Rukwa, Iringa, Njombe, Ruvuma na Mbeya. Makao makuu ya kanda hii yako hapa mjini Mbeya.

Yaliyojiri

- mbunge wa Mbeya mjini kamanda Joseph Mbilinyi alitumia fursa hiyo kuwashukuru wana Mbeya kwa kuzidi kuonyesha imani kwake na Chadema, aliwashukuru wana Mbeya kwa kuipatia Chadema ushindi wa kishindo kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya. Aliwaahidi utumishi uliotuka kutokana na upendo wa dhati wanao uonyesha kwake na Chadema.

- Mheshimiwa mbunge alitumia fursa hiyo kuwatangazia rasmi wakazi wa mjini wa Mbeya kuwa daraja la Iyela makaburini kata ya Iyela limezinduliwa rasmi baada ya serikali kukataa kiongozi wa kambi ya upinzani kulizindua daraja hilo ambalo limejengwa kwa mfuko wa jimbo kiasi cha shilingi millioni 58, akasema "...daraja hilo lingejengwa na ccm wangesema limejengwa kwa zaidi ya millioni 400.

- Kamanda Mbowe aliwapokea makada wawili wa ccm walio hamia Chadema, makada hao ni Joseph Mlozi aliyekuwa katibu wa ccm wilaya ya Makete na ndugu Okoa Mwaitenga aliyekuwa katibu mwenyezi wa ccm wa kata ya Mwakibete. Aliwakaribisha Chadema huku akiwaasa waache tabia zote chafu walizotoka nazo ccm, alizitaja tabia hizo kuwa ni Rushwa, Wizi, Ufisadi na majungu. "... Tabia hizo ni kinyume na utamaduni wa Chadema..."

- Aliongelea kuhusu uimara wa UKAWA na mpango mkakati kuelekea uchaguzi wa Oktoba, aliwaambia wana Mbeya walio furika uwanjani hapo kuwa, "... UKAWA bado uko imara sana kwa ajili ya kuwakomboa watanzania, tegemeeni wagombea bora wa UKAWA wa udiwani, ubunge na hatimae mgombea urais atakaye patikana baada ya mchakato wa ndani ya UKAWA kukamilika..."

- Mh Mbowe alitumia fursa hiyo kumuonya Mzee (Jiji) Lubuva kulinda heshima yake ili asije kuingia Kwenye historia mbaya ya kuiingiza nchi kwenye machafuko kutokana na hila ambazo tume ya uchaguzi imesha anza kuzifanya kwenye mchakato wa kuandikisha daftari la kudumu la wapiga kura. Alielezea namna tume hiyo ilivyo vunja sheria ya mwaka 1985 kama ilivyo rejewa 2010 kifungu cha 15 (1) kwa kuto boresha daftari la wapiga kura kabla na baada ya uchaguzi. Tangu 2010 baada ya uchaguzi daftari hilo halikuwahi kuboreshwa.

- Alieleza pia kuwa wataalamu wa nje walio tumiwa na tume kwenye ushauri wa kitaalamu kuhusu mfumo wa BVR wamewaandikia tume ya Taifa ya uchaguzi ripoti ambayo imebainisha kuwa tume hiyo haina uwezo wala vifaa kumudu uandikishaji wa BVR, ripoti hiyo imeeleza changamoto mbalimbali ambazo tume haiwezi kukabiliana nazo na kimsingi ni kwamba zoezi hilo limesha anza kukwama na tume na serikali hawana uwezo wa kujinasua kutokana na ukosefu wa fedha.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh Freeman Mbowe akiwahutubia mamia ya wakazi wa Mbeya waliohudhuria Mkutano Mkubwa uliyofanyika leo huko Mbeya. 


Mamia ya wakazi wa Mbeya waliohudhuria mkutano wa CHADEMA leo.

Walinzi walioshiriki kulinda mkutano wa CHADEMA Mbeya leo.

No comments:

Post a Comment