Thursday, February 12, 2015

BAVICHA wachafua hali ya hewa Bukoba, Kagasheki na Nape kwenda kujaribu kuzima moto

Na Edward Simbeye
Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA)Wamezidi kuchafua hali ya hewa Mkoani Kagera,kufuati kile kilichotegemewa na Watanzania wengi wapenda mabadidiliko kuipasua ngome ya CCM Mkoani humo.Wakati wanchama na wapenzi wa CHADEMA katika kila kona ya mji wa Bukoba wakijivunia kazi nzuri inayofanywa na vijana hao yakutoa elimu kwa watanzania hususani wananchi wa Bukoba mjini na vijijini,hali imekuwa nitofauti kwa upande wa pili wa shilingi kufuatia kutetereshwa na kuelekea kuvunjika ngome ya CCM mkoani humo.

Wakizungumza kwanyakati tofauti Makada wakongwe wa CCM Mkoani humo kwa mashariti ya kutokutajwa majina yao,wamekiri hali ya sintofahamu ndani ya chama chao tokea vijana hawa wameanza kufanya mikutano ya hadhara,Nakupata mialiko mingi ya kufanya mahojiano mbalimbali na vyombo vya habari Mkoani humo hali ya kisiasa kwa upande wao imekuwa ngumu zaidi hata kufikia baadhi ya vikao vyao kushindwa kufanyika,kwani baadhi ya wajumbe ndani ya chama wamepoteza Imani kabisa na chama cheo.

Anaendelea kusema,kama ukibahatika kuwasikiliza vijana hawa wanacho kizungumza wakiwa jukwaani,kwakweli hutamani tena kuwa ndani ya chama cha mapinduzi kwani,wanasema ukweli mtupu hawadanganyi hata kidogo.Kwakweli Serikali yetu imeshindwa kabisa kuwasidia wananchi masikini hasa sisi Wazee,tunateseka kweli kweli hatuna msaada wowote kutoka Serikalini.

Walituahidi tutatibiwa bure lakini ni uwongo mtupu ahadi zote hazijatekelezwa hata moja mpaka leo tunaelekea katika uchaguzi mkuu mwingine tena,sijui tutawaambia nini Wazee iliwatupigie kura.Kada mwingine ambae anawadhifa mkubwa ndani ya CCM,mkoa wa Bukoba nae alisema hata vikao vya jana vimeshindwa kufanyika kabisa na hivi leo tunapo zungumza tayari,Viongozi wa Wilaya wameitwa Mkoani kwenda kufanya tathimini ya namna ya kurudi kwa Wazee maana hali imekuwa mbaya zaidi.

Nae Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini,HAMISI KAGASHEKI,alipigiwa simu na wapambe wake kuelezwa hali halisi ya Jimbo kwasasa,kwakuwa haishi Bukoba nawala hana nyumba Bukoba,hivyo hajui hali ilivyo jimboni,Baada ya kupigiwa simu ameharisha kila kitu alichokuwa akikifanya nje ya Jimbo lake na huko anapoishi Jijini Dar es Salaam,haraka sana amerudi jimboni jana,kwa maandalizi ya kujipanga kuzima upepo au katika kile kinachoitwa kufukia mashimo na kuwaweka sawa wapiga kura wake,japo atakutana na upinzani mkali sana wakutokueleweka kwa wapiga kura wake,kwakuwa hakuna alichokifanya katika jimbo hilo tokea achaguliwe kuwa Mbunge.

Katika kile kinachoitwa Danganya toto HAMISI KAGASHEKI ameamua kumlipa MARLOW msanii wa muziki wa Kizazi kipya alieisha muda wake zaidi ya shilingi milioni kumi,ilikuwavutia wanachi wa Bukoba kuja kutizama shoo ya MARLOW kisha ajaribu kutupa kete yake mara tu wananchi watakapo kuja kumwangalia msanii MARLOW.Lakini pia amemualika Katibu wa itikadi na Unezi MOSES NAPE NNAUYE Kama mgeni rasmi katika mkutano huo ilikumsaidia kuweka sawa hali ya hewa,Mkutano huo utafanyika tarehe 15/02/2015.

Mashambulizi ya BAVICHA yanayoongozwa na Makamanda wanne kutoka Taifa,Makamu M/kiti Bara PATRICK OLESOSOPI,,Makamu M/kiti visiwani Zanzibar ZEUD MVANO ABDULLAHI,,N/Katibu mkuu BAVICHA bara GETRUDI KOKWENDA NDIBALEMA na EDWARD SIMBEYE Mratibuwa wa uhamasishaji BAVICHA Taifa,ambaepia ni msemaji wa Baraza,yamewafanya CCM mkoani Kagera kuwa katika wakati mgumu sana,Viva BAVICHA vivaaaaaaaaaaaa.

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki CHADEMA.

No comments:

Post a Comment