Saturday, July 12, 2014

TANZANIA NAMNA HII, MALIASILI NA UTALII UKO SHAKANI

Hii ndiyo video ambayo Mheshimiwa Peter Msigwa (MB), Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, aliiwasilisha ndani ya bunge kama sehemu ya ushahidi wake akionesha namna ambavyo Serikali ya CCM inaachia vitendo vya kijangiri/uwindaji haramu kufanyika mchana kweupe bila hatua kuchukuliwa.

Pamoja na Msigwa kuwasilisha ushahidi huo bungeni ili wahusika wachukue hatua stahiki, bado Serikali ya CCM imekuwa butu. Jana akaamua kuiweka hadharani video hiyo mbele ya waandishi wa habari, ili hatimaye umma wa Watanzania uone namna ambavyo sekta ya wanyama pori hatimaye itaangamizwa kwa sababu tu ya UFISADI wa walioko madarakani.

Jionee mwenyewe. Hapo chini kuna docs mbili muhimu, sehemu ya press release ya Peter Msigwa aliyoitoa jana kwa waandishi wa habari. 

Pia kuna doc inayoonesha namna ambavyo wahusika wamefanya makosa 11 kwa kuvunja sheria za nchi na zile za kimataifa zinazoruhusu uwindaji wa kisheria, lakini jamaa bado wako nchini wakitamba na kuharibu uchumi wetu kupitia maliasili na utalii, kadri wanavyotaka wao.


No comments:

Post a Comment