Thursday, May 1, 2014

MKUTANO WA UKAWA KIBANDA MAITI ZANZIBAR

Viongozi wa Wajumbe wa kundi la UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi) ndani ya Bunge Malaum la Katiba, wamehutubia maelfu ya watu waliohudhuria mkutano wao katika viwanja vya Kibanda Maiti mjini Unguja, Zanzibar jioni ya leo.

Aidha, katika mkutano huo katika mkutano ilielezwa kuwa ushirikiano wa UKAWA sasa siyo katika katiba pekee bali utakuwa mpaka Bungeni ambapo wanatarajia kuivunja Serikali ya sasa kivuli na kuunda nyingine yenye wajumbe mchanganyiko kutoka katika vyama mbalimbali.

Kwa mujibu wa Katibu wa UKAWA ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, mkutano mwingine wa UKAWA unatarajiwa kufanyika Pemba hapo kesho kabla ya mikutano kama hiyo kuendelea katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara/Tanganyika kama vile Dar es Salaam, Kigoma, Morogoro, Mwanza, Iringa, Arusha n.k.

Mtatiro amesema lengo la mikutano hiyo ni kuwaelimisha wananchi juu ya hatua yao ya kuondoka Bungeni na kususia vikao vya Bunge Maalum la Katiba na kile wanachoamini kinapaswa kufanyika.

Katibu mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa (Kulia) Akihutubia mamia wa wakazi wa Zanzibar katika kiwanja cha Kibanda Maiti. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad.

Mami ya Wakazi wa Zanzibar waliojitokeza katika Mkutano wa Ukawa Zanzibar.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akipeana mkono na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mh Maalimu Seif Shariff Hamad.






No comments:

Post a Comment