Thursday, March 27, 2014

M/Kiti Bunge la Katiba aahirisha kikao: Kanuni hizi hazijadiliki, hazipiti!

Maelezo ya Bi. Salma Said, Mjumbe wa Bunge la Katiba -- Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba hawajaridhishwa na mwenendo wa Mwenyekiti wa Bunge hilo Samweli Sitta namna anavyoendesha vikao na kukiukwa baadhi ya kanuni za bunge hilo, Mjumbe wa Bunge hilo Tundu Lissu leo alionesha kutoridhishwa kwake na kusema kanuni zilizobadilishwa hazijadiliki wala hazipiti.

Naye Abubakar Khamis Bakar alisema haiwezekani bunge likakiuka kanuni na wajumbe wakaendelea kunyamaza kimya.

Ismail Jussa alihoji kwa Mwenyekiti wa Bunge hilo kwamba kanuni zilizotungwa na kuridhiwa na wajumbe wote vipi
kabla hata kuanza kazi zifanyiwe marekebisho bila hata ya kufuata utaratibu unaokubalika? Alisema hawatakubali kujadiliwa kwa kanuni yoyote kati ya hizo kwa kuwa hazijadiliki katika kikao hicho kwa pamoja walisema hawatakubaliana kujadiliwa kwa kanuni hata moja kati ya hizo zilizobadilishwa wakisema hazijadiliki wala hazipiti.

Mwenyekiti akalazimika kuahirisha kikao cha Bunge hilo hadi kesho saa 10 jioni, hali iliyowakasirisha baadhi ya Wabunge wa Bunge hilo.

JEDWALI LA MAREKEBISHO KATIKA KANUNI ZA BUNGE MAALUM

Kanuni za bunge zinafanyia marekebisho kama ifuatavyo:

A. Kanuni ya 14. (1) inafanyiwa kwa:

(a) kufuta neno jumamosi na badala yake kuweka neno alhamisi.

(b) kwa kuongeza fasili mpya ya (4) kama ifuatavyo:

“(4) Bunge Maalum kwa siku za Jumamosi litakutana kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana ambapo Mwenyekiti ataakhirisha shughuli za Bunge Maalum hadi Jumatatu”.

(c) kwa kupanga upya fasili ya (4) hadi ya (9) kuwa fasili ya (5) hadi (10).

B. Kanuni ya 32 inafanyiwa marekebisho kwa:

(a) Kufuta fasili ya (1) na ya (2) na kuziandika upya kama ifuatavyo:
(b) kuandika upya fasili ya (1) kama ifuatavyo:


(1) kila kamati itajadili rasimu ya katika kwa wakati mmoja kwa kuzingatia mgawanyo wa sura za rasimu ya katiba kwa mujibu wa muda na ratiba itakayopangwa na kamati ya uongozi.

(2) utaratibu wa kuendesha mijadala katika kamati utakuwa kama utaratibu katika bunge maalum kwa mujibu wa kanuni hizi.

C. Kanuni ya 33 inafanyiwa marekebisho kama ifuatavyo:

(a) kwenye fasili ya (5) kwa kuongoza maneno ya nyongeza kama ifuatavyo:
“Isipokuwa kama maoni ya walio wachache yanatofautiana, Mwenyekiti anaweza kumruhusu Mjumbe mwingine miongoni mwao kutoa ufafanuzi unaohitajika kuhusu jambo husika ndani ya muda uliopangwa katika fasili hii”,
(b) kwenye fasili ya (7), kwa kufuta maneno “kipindi kisichozidi siku tatu” na kuweka badala yake maneno “muda utakaopangwa na kamati ya uongozi”;
(c) kwa kuifuta fasili ya (10) na kuweka badala yake fasili mpya ifuatayo:
(10) katika kuchangia mapendekezo kwa mujibu wa fasili ya (9),

Mwenyekiti atatoa nafasi kqa Wajumbe kwa idadi ambayo Mwenyekiti ataona inafaa badala ya kuzingatia uzito na umuhimu wa mapendekezo ya marekebisho, maboresho au mabadiliko yaliowasilishwa na Mjumbe husika”.

D: Kanuni ya 35 inafanyiwa marekebisho:

(a) kwenye fasili (6) kwa kufuta neno “mbili” yaliyopo katika mstari wa kwanza wa fasili hiyo;


(b) kwenye fasili ya (8), kwa kuingiza baada ya neno “Mwenyekiti”, maneno “kwa kushauriana na kamati ya uongozi”: E: kanuni ya 58 (1)(d) inafanyiwa marekebisho kwa kufuta neno “watano” na kuweka badala yake neno “saba”.

F: Kanuni ya 63 (1) inafanyiwa marekebisho kwa kufuta maneno “kwa kuzingatia muda uliowekwa na sheria” na badala yake kuweka maneno “kwa kadri watakavyoona inafaa”.

G. Kanuni ya 64 inafanyiwa marekebisho.

(a) kwa kufuta fasili ya (1) na kuiandika upya kama ifuatavyo:

64. (a) bila ya kuathiri masharti ya sheria na kanuni hizi utaratibu wa kamati kufanya uamuzi utakuwa ni kwa Mwenyekiti wa kamati kuihoji kamati na kupata uamuzi wa wajumbe utakaotokana na wingi wa idadi ya wajumbe kwa mujibu wa masharti yakiowekwa na kanuni hizi:

Isipokuwa kwamba, ili ibara au rasimu ya katiba iweze kupitishwa katika kamati itahitajika kuungwa mkono kwa wingi wa thuluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote wa kamati kutoka Tanzania Zanzibar ya idadi ya wajumbe wa kamati kutoka Tanzania Bara na

(2) Uamuzi chini ya fasili ya (1) hata kama haukufikia theluthi mbili suala hilo litapelekwa kwenye bunge maalum.

(b) kupanga upya fasili ya (2) hadi ya (5) kuwa fasili ya (3) hadi ya (6). 1

Kanuni ya 85 inafanyiwa marekebisho kwa kuifuta fasili ya (4).

No comments:

Post a Comment