Friday, February 21, 2014

Chadema yamvua Uongozi Katibu wa Wilaya kwa Usaliti.

KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Mvomero, imedaiwa kumvua Uongozi Katibu wa Wilaya wa Chama hicho hicho wilayani humo, Mrisho Ramadhani, kwa madai ya kukisaliti Chama.
Habari toka ndani ya kikao cha siri kilichoketi Ofisi ya Wilaya zinadai, Kamati ilimvua ukatibu Mrisho kutokana na kufanya maamuzi ya kukiunganisha Chadema na Vyama vingine bila ridhaa ya Chama, na kumdharilisha Diwani wake, Luka Mwakambaya.
Akizungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina Mtoa habari wetu alisema, Mrisho amebakiwa na Ukatibu Mwenezi wa Wilaya, amabapo suala lake limepelekwa kwenye Mkutano Mkuu akajadiliwe na kutolewa maamuzi.
“Baada ya Chadema kutangaza kufanya mkutano wa M4C–Opresheni ya Pamaoja Daiama (OPD) Kata ya Mtibwa 29.1.2014, Mrisho aliacha Sera za Chadema za kutatua kero za wakulima na wafanyakazi zilizofanywa na Mwakambaya na kuungana na wanaokwamisha OPD.
“Kama haitoshi, 29.1.2013, alimdharilisha Diwani wa Kata ya Mtibwa, Mwakambaya (Chadema) katika Mkutano hadhara, akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe, aliyetaka aelewe Kero za Mwekezaji wa Mtibwa aende nazo bungeni”.alisema mtoa habari.
Mkutano huo Mrisho alisema, ‘kutokana na kero za mwekezaji wa Mtibwa kukithiri akiwacheleweshea malipo Wakulima wa wadogo wa miwa na wafanyakazi, Chadema kimeungana na Vyama vingine kudai haki kwa maandamano baada ya Diwani Mwakambaya kushindwa, jambo ambalo halikuwa kweli na lilipingwa na wananchi, kwa sababu amekuwa akilala langoni mwa lango la mwekezaji na kulazimika kuwalipa.
Aidha baada ya gazeti hili kumtafuta Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mvomero Saimanga Kashikashi bila mafanikio, lilimtafuta Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Msingi Chadema, Innocent Zawadi kutaka kujua suala hilo, naye alisema ngoja awasiliane na uongozi wa Wilaya ya Mvomero kupata habari sahihi.
Nafasi ya Katibu wa Wilaya ya Mvomero (Chadema) tangu uchaguzi ufanyike, imekuwa ikipyaya na kukaimishwa kwa mara pili sasa, ambapo baada ya kikao hicho jana imekaimishwa kwa, Rosemaary Kimune, huku wapenzi wa Chadema wakikitaka chama kutafuta mtu makini.

No comments:

Post a Comment