CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Waziri wa Fedha na Uchumi na Mbunge wa Kalenga, Dkt. William Mgimwa ambaye amefariki akiwa kwenye matibabu Afrika Kusini.
Kwa masikitiko makubwa CHADEMA kinatuma salaam za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwa kuondokewa na msaidizi wake wa karibu na mtumishi mwenzake serikalini.
Chama kinatoa salaam za dhati kwa familia ya marehemu Mgimwa kwa kuondokewa na baba na mpendwa wao, katika wakati ambao tunaamini walikuwa bado wakimhitaji sana kama moja ya nguzo za familia.
CHADEMA pia inatuma salaam za pole kwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na msiba huo wa kuondokewa na mmoja wa wanachama na wabunge wake.
Mwenyezi Mungu awapatie moyo wa subira wakati huu wa majonzi mazito ya kuondokewa na mpendwa wao, Dkt. Mgimwa.
Kurugenzi ya Habari
No comments:
Post a Comment