Sunday, January 19, 2014

Chadema Kongwa yamrushia Ndugai Zigo la Vifo vya Wakulima Kiteto.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Kongwa, kimemrushia zigo la vifo vya wakulima Kiteto Mbunge na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, kwamba alikuwa sababisho la vifo vya watu waliouawa kinyama, kwa kuwatumainisha waende wakalime.

Hayo yamesemwa jana na Mwenyekiti wa Chadema wilayani humo, Juma Chibiriti, alipoliaambia gazeti hili sababu za kutokea kwa vifo vya wakulima hao, ambapo pia kilihusisha kifo cha Mchungaji na Mwanae wa Kata ya Ngomai, waliouawa kinyama.

Akizungumza na mwandishi Chibiriti alisema, katika Mkutano wa hadhara alioufanya Ndugai Mji Mdogo wa Kibaigwa hivi karibuni, aliwatumainisha wakulima waende kulima katika maeneo hayo  badala ya kuwatahadharisha kutokana na hali mbaya ya sintofahamu iliyokuwepo.

”Binafsi nilimweleza Ndugai juu ya Kauli aliyoitoa Kibaigwa, kwamba inaweza kusababisha athari, lakini nikapuuzwa, hivyo wakulima walioichukuwa kauli ile kuwa imezungumzwa na mtu mwenye mamlaka ya Kibunge, matokeo yake, sasa tumepoteza Nguvu Kazi pasipo na sababu.

Chibiriti alisema, ‘Kauli hiyo Ndugai aliirudia tena kwenye kijiji cha Ngomai wakati wa mazishi ya Mchungaji na Mwanae, na aliongeza kwamba, kuwataka wananchi wakajiandikishe ili kuwangoa viongozi wa Kiteto, haiwapi wananchi tabia ya kutunza Amani nchini’.

Mwenyekiti wa Chadema Kongwa (Chibiriti), amewaasa wananchi wa Kongwa wanaofanya kazi ya Kilimo Kiteto, kwa sasa watulie wasing’nganie kulima huko hadi Serikali itakapomaliza Utata uliopo kati ya wakulima na wafugaji, baada ya kumalizika kwa kesi mahakamani, ili kulinda maisha yao.

Awali baada ya kutokea kutoelewana kati ya wakulima na wafugaji kiteto, Ndugai alifanya Mkutano Mji Mdogo wa Kibaigwa, ambapo Chibiriti anadai aliwatumainisha wakulima wa Kongwa wanaolima Kiteto, waendelee kulima huko ingawa amani yake haikuwa nzuri.

No comments:

Post a Comment