Saturday, December 21, 2013

Waziri Kagasheki atangaza kujiuzulu; Rais Kikwete awafuta kazi Mawaziri wanne

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki ametangaza Bungeni kuwa amejiuzulu kutoka katika wadhifa wake huo kutokana na Ripoti ya Kamati iliyoundwa kuchunguza madhila yaliyotokana na Operesheni Tokomeza Ujangili, operesheni iliyotekelezwa na Wizara yake ikishirikiana wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Kagasheki alitoa kauli yake hiyo na kusema kuwa anapaswa kuwajibika, mara tu alipozungumza baada ya Wabunge

kuchangia hoja hiyo iliyotikisa Bunge na kuleta simanzi kubwa kutokana na unyama uliofanywa dhidi ya wananchi ikiwemo kuteswa, kubakwa kwa wanawake na wengine kuuawa, adha iliyoikumba pia mifugo. , Kagasheki alisema anapaswa kuwajibika.

Taarifa zaidi za Bungeni zimesema kuwa Rais Kikwete amepokea ripoti husika na kuridhia kuwafuta nafasi za uwaziri mawaziri wanne.

Uamuzi huo ambao umesomwa na Waziri Mkuu, Mizengo PInda umewataja mawaziri waliofutwa kazi kuwa ni Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vua Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Mathayo David Mathayo (MIfugo na Uvuvi) na Hamisi Kagasheki (Mali asil na Utalii).

1 comment:

  1. Kujiuzulu si suluhisho la maumivu ya Watanzania. Wanaumizwa wengi tena kwa kutumia gharama za kodi zao harafu watu wanne tu wanajiuzulu! Yafaa ufuatiliaji wa moja kwa moja dhidi ya watesaji kwa kuwa wanafahamika ili kujua kama walitumwa au ni Umungu wao.

    Pia, naomba huyu mkuu wa kaya asithubutu kuwapa majukumu mengine hawa vijana wake wanne ili kuondoa dhana ya maigizo katiaka historia ya kujiuzulu.

    SWALI; Kwaninini mnyamapori akiathiri makazi ya watu huswagwa kuelekezwa porini lakini binadamu akiathiri porini husulubiwa kifo na anayegoma kufa hulazimishwa kuishi gerezani?

    ReplyDelete